Header Ads Widget

WAKALA WA VIPIMO SHINYANGA WAWASHAURI WAFANYABIASHARA

Afisa vipimo mkoa wa Shinyanga akitoa elimu kwa wauza mchele Ibinzamata

Na Kareny Masasy,
Shinyanga,

WAKALA wa vipimo (WMA) mkoani Shinyanga wamewashauri wafanyabiashara kuweka nembo kwenye vifungashio ili kuweza kutambulika kisheria kwa Usalama wao na bidhaa wanazozisindika.

Hayo yamesemwa leo Jumamosi Mei 20,2023 na Afisa vipimo mkoa wa Shinyanga Happiness Saronge wakati Akiongea na wafanyabiashara wa Michele eneo la Ibinzamata manispaa ya Shinyanga katika kuazimisha siku ya vipimo duniani yenye kauli vipimo vinavyotumika kwenye mfumo wa chakula duniani.

Saronge amesema leo wanatoa Elimu ya vifungashio Wafanyabiashara wanatakiwa wawe na nembo ili ijulikane imetengenezwa lini,muda wa kuisha matumizi yake na vipimo vilivyomo kama ni sahihi.

"Wafanyabiashara kila mwaka wanatakiwa kugaguliwa mizani zao lengo lake ni kuona kama inapunja mteja au kujipunja na mwenye mizani mpya wahakikishe inakaguliwa wapo wanaofanya udanganyifu katika kufungasha"amesema Saronge.

Saronge amewataka wanaofungasha waweke pia majina yao kwa kutumia mashine sio kwa kuandika na Mark pen hilo ni kosa kisheria na mteja akija analalamika kupewa mfuko wa bidhaa pungufu bila Nembo hatasikilizwa sababu hawatatambua anamlalamikia nani.

Saronge amesema marekebisho ya mzani yanafanyika kwa gharama kidogo kwa kutofautisha aina ya mizani aliyonayo mfanyabiashara huku akiwashauri wazitumie vipimo vya madebe au Sado kupima bidhaa watumie mizani.

Baadhi ya wafanyabiadhara waliohufhuria utolewaji wa Elimu hiyo akiwemo Joel Albert amesema Wakulima vijijini wao wenyewe wanapenda kutumia vipimo vya ndoo wakienda na mizani wanazikataa kwa kudai hawaziamini zimechakachuliwa.

Ezeckiel Mabala amesema wao ni wafanyabiashara wanao uza kwa rejareja kuweka nembo itakuwa ni ngumu sababu hawatumii vifungashio mteja anakuja moja kwa moja mashineni kuchukua mchele akiwa na kifungashio chake.


Aidha wafanyabiashara kwa pamoja waliomba Wakala wa vipimo inapifika wakati wa ukaguzi mizani waende moja kwa moja kwenye maeneo yao walipo siyo kwenye ofisi za watendaji wa kata unakuwa ni usumbufu.
Afisa vipimo mkoa wa Shinyanga akitoa elimu kwa wauza mchele Ibinzamata
Wafanyakazi wa wakala wa vipimo mkoa wa Shinya wakitoka kwenye zoezi la kutoa elimu
Afisa vipimo mkoa wa Shinyanga akitoa elimu kwa wauza mchele Ibinzamata
Afisa vipimo mkoa wa Shinyanga akitoa elimu kwa wauza mchele Ibinzamata
Afisa vipimo mkoa wa Shinyanga akitoa elimu kwa wauza mchele Ibinzamata

Post a Comment

0 Comments