
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni naibu waziri ofisi ya Waziri mkuu kazi, vijana na ajira akizungumza kwenye mafunzo ya UWT wilaya
Suzy Luhende,Shinyanga Blog
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni naibu waziri ofisi ya Waziri mkuu kazi, vijana na ajira, amewagiza maafisa elimu wa shule ya sekondari na msingi kufanye ziara mashuleni ili kujua kama kweli michango wanayotumwa wanafunzi ipo kisheria.
Agizo hilo amelitoa leo alipokuwa mgeni rasimi kwenye mafunzo ya wajumbe wa baraza la Umoja wa Wanawake Tanzania UWT wilaya ya Shinyanga mjini iliyokuwa ikiwahusu wenyeviti na makatibu wa UWT kata, matawi na makatibu wa CCM kata kutoka wilaya ya Shinyanga mjini kwa ajili ya kujiimarisha.
Katambi amesema amepata malalamiko kwa wazazi kuwa michango imezidi kwa wanafunzi na huku serikali imetoa fedha kwa ajili ya elimu ya sekondari na msingi zaidi ya sh 844 milioni, hivyo kuna elimu bila malipo kwa wanafunzi wote wanaosoma shule za serikali.
"Nimeambiwa kuna michango mingi sana inafanyika kwenye shule zetu wananchi wanalalamika, hivyo afisa elimu sekondari na afisa elimu msingi niwaombe mfanye ziara mashuleni ili muweze kuja kutoa ufafanuzi kuhusiana na michango hii,"amesema Katambi.
"Kazi ya Chama Cha Mapinduzi CCM na jumuia zake, kazi yake ni kusimamia miradi mbalimbali ya Chama Cha Mapinduzi CCM na kutatua kero mbalimbali zilizopo kwenye jamii, hivyo mmefanya vizuri kulileta suala hili hapa ili liende likatatuliwe na watoto waendelee na masomo kwa amani, ameongeza Katambi.
Katika hatua nyingine mwenyekiti wa UWT mkoa wa Shinyanga Grace Samweli amesema lengo la mafunzo hayo ni kuimarisha umoja wa wanawake ili waweze kusimama imara katika uongozi na kujua itifaki za uongozi, pamoja na kufanya kazi kwa maadili yanayotakiwa.
"Niwaombe ndugu zangu wanawake mkayafanyie kazi haya yote mliyofundishwa katika utendaji kazi wenu mkaheshimiane mkubwa kwa mdogo, kinachotakiwa kila mmoja asimame kwenye nafasi yake na kila mmoja ajue majukumu yake ya kikazi ,"amesema Samweli.
Naye mjumbe wa baraza la UWT Taifa Christina Gule amewashauri wanawake wafanye kazi kwa bidii, lakini wasiwasahau watoto wao kuwafundisha maadili mema wasikimbilie kwenye vikoba na kuwaacha wakifundishana vitu visivyofaa kwenye jamii.
Katika mafunzo hayo zilifundishwa maada mbalimbali ikiwemo mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto, sheria haki na wajibu, majukumu muhimu ya uongozi, itifaki na utaratibu, nafasi ya UWT kuelekea uchaguzi, mkakati wa UWT wa kuimalisha Chama, nafasi ya uongozi na watendaji na mwelekeo wa UWT
Kwa upande wake mwenyekiti wa UWT wilaya ya Shinyanga Rehema Nhamanilo amewashukuru wanawake wote kwa kuhudhulia mafunzo hayo ambayo yatawasaidia katika kufanya shughuli zao za jumuia, hivyo amesema mafundisho waliyoyapata wakayafikishe kwenye matawi ili kila mmoja atambue majukumu yake.



Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akitoa elimu juu ya masuala mbalimbali ya uongozi


Katibu wa UWT mkoa wa Shinyanga Asha Kitandala akizungumza na viongozi wa UWT wilaya ya Shinyanga

Katibu msaidizi wa mkoa wa Shinyanga Halima Makologanya akizungumza kwenye mafunzo ya UWT ambapo aliwaomba wanawake waendelee kumuunga mkono Rais Samia Suluhu




Katibu wa UWT wilaya ya Shinyanga Lucy Enock akizungumza kwenye mafunzo hayo


Afisa uchumi na biashara akitoa maada za uchumi kwa wanawake bapo aliwaomba wawe na miradi mbalimbali kuanzia wilaya kata hadi matawi




Jane Mwanzembe kutoka dawati la jinsia wilaya ya Shinyanga akitoa maada ya ukatili wa kijinsia kwenye semina ya UWT Wilaya ya Shinyanga







Viongozi mbalimbali wa UWT wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa wilaya

Viongozi mbalimbali wa UWT na makatibu wa kata CCM wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa wilaya



