Header Ads Widget

TUME YA TAIFA UNESCO KUENDELEA KUSHIRIKIANA NA MISA-TAN KUCHECHEMUA UHURU WA KUJIELEZA

Tume ya taifa ya UNESCO kuendelea kushirikiana na Misa-Tan kuchechemua Uhuru wa kujieleza

Na Marco Maduhu, DODOMA

TUME ya Taifa ya UNESCO, imeahidi kuendelea kushirikiana na Taasisi ya vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika Tawi la Tanzania (MISA-Tanzania), katika kuhamasisha uhuru wa kujieleza, uhuru wa habari na upatikanaji habari.

Mwakilishi wa Tume ya Taifa ya UNESCO Festo Suzubeki, amebainisha hayo leo Mei 26.2023 katika siku ya Pili ya Maadhimisho ya miaka 30 ya kuanzishwa kwa MISA, yalioendana sambamba na majadiliano ya mada mbalimbali ambazo zinahusu changamoto zinazoikabili sekta ya habari na kuzitafuta ufumbuzi.

Amesema UNESCO katika kitengo cha Sekta ya Habari na Mawasiliano, majukumu ambayo wamekuwa wakiyafanya ni kuhamasisha uhuru wa kujieleza, uhuru wa habari, na upatikanaji wa habari, jukumu ambalo limekuwa likifanywa pia ni Misa-Tanzania, na kuahidi kuendelea kushirikiana sababu habari ni muhimu katika Maendeleo ya Taifa.

“UNESCO na MISA sisi ni ndugu, sababu tunatekeleza majukumu ya kuhamasisha uhuru wa kujieleza, uhuru wa habari na upatikanaji wa habari tuna ahidi kuendelea kushirikiana na ninyi katika masuala ya habari kwa ajili ya maendeleo ya Taifa, na tunawapongeza kwa kutimiza miaka 30,”amesema Suzubeki.

Katika hatua nyingine, amewakaribisha MISA kutumia fursa mbalimbali ambazo wanazo UNESCO, kwa kuandika maandiko na kupata fedha ambazo zitawasaidia katika utekelezaji wa majukumu yao na kuhamasisha uhuru wa kujieleza.

Aidha, Misa-Tanzania ilianzishwa mwaka 1993, baada ya kikao cha Wanahabari waliokutana Windhoek, Namibia kujadili mambo mbalimbali yaliyokuwa yanaukabili Ukanda wa Nchi za Kusini.

Kwa mwaka huu (2023) MISA Tanzania ina adhimisha miaka 30, kwa kufanya kazi ya kichechemuzi katika uhuru wa habari, uhuru wa kujieleza, kupata na kutoa taarifa.

Kauli Mbiu katika maadhimisho ya miaka 30 ya MISA-Tanzania mwaka huu (2023) inasema “Uhuru wa kujieleza msingi wa haki kwa maendeleo endelevu.”
Mkurugenzi wa Misa-Tanzania Elizabeth Riziki akizungumza kwenye siku ya Pili ya Maadhimisho ya miaka 30 ya MISA yaliyoendana sambamba na majadiliano ya changamoto ambazo zinaikabili sekta ya habari na kuzitafutia ufumbuzi.
Mwenyekiti wa MISA-Tanzania Salome Kitomari akizungumza kwenye mkutano huo ulioendana sambamba na Maadhimisho ya miaka 30 ya MISA.
Mwakilishi wa Tume ya Taifa ya UNESCO Festo Suzubeki, akizungumza kwenye siku ya pili ya maadhimisho ya miaka 30 ya MISA-Tanzania.
Mwenyekiti wa MISA-Tanzania Salome Kitomari akichukua kumbukumbu.
Wanachama wa MISA-Tanzania wakiendelea na mkutano ulioambatana na maadhimisho ya miaka 30 ya MISA.
Wanachama wa MISA-Tanzania wakiendelea na mkutano.
Wanachama wa MISA-Tanzania wakiendelea na mkutano.
Wanachama wa MISA-Tanzania wakiendelea na mkutano.
Wanachama wa MISA-Tanzania wakiendelea na mkutano.
Wanachama wa MISA-Tanzania wakiendelea na mkutano.
Wanachama wa MISA-Tanzania wakiendelea na mkutano.
Wanachama wa MISA-Tanzania wakiendelea na mkutano.
Wanachama wa MISA-Tanzania wakiendelea na mkutano.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Wanachama wa MISA-Tanzania wakiendelea na mkutano.

Post a Comment

0 Comments