Header Ads Widget

WEADO NA WADAU WAFANYA KIKAO CHA TATHIMINI YA MRADI WA VUNJA UKIMYA, ZUIA NDOA NA MIMBA ZA UTOTONI –HALMASHAURI YA WILAYA YA SHINYANGA.


WEADO NA WADAU WAFANYA KIKAO CHA TATHIMINI YA MRADI WA VUNJA UKIMYA, ZUIA NDOA NA MIMBA ZA UTOTONI –HALMASHAURI YA WILAYA YA SHINYANGA.

Na mwandishi wetu.

Wadau wa kutokomekeza ukatili kutoka Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga wamefanya kikao cha tathimini ya mradi wa kutokomeza mimba na ndoa za utotoni unaotekelezwa  shirika la WEADO(Women Elderly Advocacy and Development organization) katika kata za masengwa na tinde kwa  ufadhili wa Foundation For Civil   Society.

Kikao hicho kimefanyika leo machi 25,2023 kwa kuongozwa na Mgeni Rasmi Nuru Yunge,Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga aliyeambatana na Mratibu wa dawati la jinsia na watoto jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga , Mrakibu mwandamzi ,Monica Sehere.Kikao hicho kimefanyika kwa ajili ya kujadili mrejesho wa utekelezaji wa mradi wa awamu ya kwanza wa  VUNJA UKIMYA,ZUIA NDOA NA MIMBA ZA UTOTONI unatekelezwa kwa kipindi cha septemba,2022 hadi Aprili,2023,ambapo taarifa za mafanikio,changamoto na matokeo yaliwasilishwa kwa wadau walioshiriki katika mradi huo.

Kikao hicho kiliweza kuhudhuriwa na makundi mbalimbali ikiwa maafisa maendeleo jamii,waratibu elimu kata,maafisa ustawi,viongozi wa dini,majukwa ya wanawake, polisi kata,wazee wa mila na wakililishi kutoka mabaraza ya watoto kutoka kata ya tinde na masengwa.

Mkurugenzi wa Shirika la WEADO,Eliasenya Nnko ,anasema suala la kutokomeza ukatili linahitaji nguvu ya pamoja kwa ajili ya kusaidia wanawake na watoto kwa kuwa bado mila na desturi zimekuwa ni changamoto kwa kutoa haki kwa wanawake na watoto wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Hali ya kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto ,inahitaji nguvu ya pamoja na tuko hapa kupeana tathimini ya mwelekeo tulionao na kuweza kuwa na mikakati mingine kwa pamoja”Anasema Eliasenya.

Akifungua kikao, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Shinyanga, Nuru Yunge alisema,Halmashauri hiyo bado ina changamoto za masuala ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto na ninashukuru wadau wanaotekeleza miradi ili kusaidia kutokomeza ukatili katika Halmashauri yetu.

Kikao hiki ni muhimu kwetu sote ili tuweze kupata mazuri ambayo tuyafanyia kazi  na kuweza kuweka mikakati imara ili tuweze kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto kabisa si kupunguza tu”Anasema Nuru

Aidha,Nuru alisema Halmasahuri hiyo inati takwa la kisheria la kutoa mikopo kwa wanawake na vijana kwa asilimia 10 kama serikali inavyotaka na ni fursa kwa wanawake wa Halmashauri hiyo ,Hivyo hawapaswi kuogopa.

Kwa upande wa uwasilishaji wa taarifa za wadau waliwasilisha taarifa za mafaniko na changamoto kwa kila kundi.

Afisa Maendeleo jamii kata ya tinde na masengwa ,walisema wanawake wamevunja ukimya na wanaweza kuripoti kwa sasa baada ya elimu na hata kutoa huduma kwa watoto wa mazingira magumu kwa rasilimali zao

“Wanawake wa hapa masengwa walishirikiana kwa pamoja kutoa taarifa katika ofisi yangu kwa mwanamke aliyepigwa na mme wake”Anasema Atupile Maseta-Afisa maendeleo kata Masengwa.

“Wanawake wanatoa maziwa na kumtembelea mtoto anayeishi mazingira magumu” Eva E. Mlowe-Afisa maendeleo jamii kata ya tinde.

Waratibu wa elimu kata wanasema hakuna suala la mimba na ndoa za utotoni kwa kipindi cha desemba,2022 hadi machi,2023 kwa kata za masengwa na tinde kwa kuwa mabaraza ya watoto yametumika kutoa elimu.

Viongozi wa dini wa kata ya tinde na masengwa walisema,wameweka mkazo zaidi juu ya usajili wa watu we ye sifa na vigezo vya kufunga ndoa na wametoa elimu hiyo kwa waumini.

“sheria ya dini ya uislamu inaruhusu msichana wa miaka 14 kufungishwa ndoa,ila kwa kupitia elimu ya WEADO,tulielimisha viongozi wa msikiti ya vitongoji na kuweka zuio la ndoa za mikeka kwa wasichana chini ya miaka 18” Hemed Rashid-Shehe wa kata ya tinde.

Ndani ya jumuiya zetu,tumetoa maelezo ya vigezo Maalum vya wanaostahili umri sahihi wa kuandikisha ndoa”Esta Eliya-Katekista –Busanda.

Upande wa jukwa la wanawake wa kata za tinde na masengwa,walisema mradi umesaidia kuinua kiuchumi na kuwapa ujasiri wa kujitetea juu ya haki zao.

“Nilitelekezwa na kuachiwa watoto tisa(9) na niliishi mazingira magumu ya uchumi,WEADO wamenisaidia na leo wanafundisha wanawake wenzangu kujikwamua kiuchumi”Sarah Mayunga-Katibu jukwa la wanawake tinde.

Wakilishi wa baraza la watoto kata ya tinde na masengwa wanasema,tumefundisha wenzetu kutoa taarifa za vitendo vya ukatili kwa waalimu na kupiga namba 116 kupitia mabaraza ya watoto.

Watoto wameweza kubaini vitendo vya ukatili majumbani na wana ujasiri wa kusema”Mayenga Mabula-Masengwa shule ya msingi.

Kadhalika, Afisa wa dawati la jinsia kituo cha polisi tinde,Norbert Boniface anasema hawajapokea kesi ya mimba na ndoa za utotoni kwa kipinidi cha janauri hadi machi,2023 ila changamoto ni wazazi na walezi kutokuwa na ushirikiano na jeshi la polisi.

Mratibu wa Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Shinyanga, Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi, Monica Venance Sehere,akitoa neno kwa niaba ya jeshi la polisi ,anasema hawajapokea kesi za mimba na ndoa za utotoni kwa kata za tinde na masengwa kwa januari hadi machi,2023 ila changamoto kubwa ni jamii kuchelewa kutoa taarifa kwa jeshi la polisi.

Katika upande mwingine,Happyness Misael, Msajili Msaidizi wa mashirika yasiyo ya kiserikali,akitoa shukrani zake ,alisema ni muhimu kuboresha na mfumo mzuri wa kutoa taarifa za kesi za ukatili na kujua za mrejesho wa kesi zinazofikisha Vyombo vya dola ili kurudisha matokeo kwa jamii ili kuweza kuisukuma kushiriki zaidi.

Joram Magana,Afisa maendeleo jamii wilaya ya Shinyanga ,alishukuru shirika la WEADO kwa kusema wamefanikiwa kuwa na matokeo ya kutokuwepo kwa mimba na ndoa za utotoni kwa kata hizo mbili na kuwataka wadau wote kuweza kuwa na matokeo  chanya kwa kata zingine 24 za halmshauri hiyo.


Mkurugenzi wa shirika la WEADO,Eliasenya Nnko akizgumza kuhusu lengo la kikao hicho.


Mratibu wa Dawati la Jinsia na Watoto Mkoa wa Shinyanga, Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi, Monica Venance Sehere,akizungumza kuhusu kesi za mimba na ndoa za utotoni.
CPL.Norbet Boniface wa kituo cha polisi tinde kitengo cha dawati la jinsia akitoa taarifa ya hali ya kesi za  ukatili .

John Eddy,meneja wa shirika la WEADO akitoa maelekezo juu ya ushiriki wa kikao.

Afisa mradi wa vunja ukimya,zuia ndoa na mimba za utotoni,Winnie Hinaya akielezea kuhusu utekelezaji wa mradi.

Esta Eliya katekista wa parokia ya busanda akizunguzma juu ya utoaji elimu kwa dini kuhusu ndoa na masuala ya kuthibiti vitendo vya ukatili.

Juma chiamba,mratibu elimu kata ya masengwa akizungumzi jinsi wanavyothibiti ndoa na mimba za utotoni.

Mratibu elimu kata ya tinde.

Mzee wa kimila na chifu Thomas Kipela kutoka kata ya tinde akizungumzia umuhimu wa kushirikisha wazee wa kimila katika afua za kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.


Hoka jitulu,Mwakilishi jukwaa la wanawake kata ya masengwa akiwasilisha taarifa ya utekelezaji.
Mayenga Mabula mwakilishi wa baraza la watoto shule ya msingi masengwa akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa baraza la watoto.

Alfred Kasanzu mwakilish wa baraza la watoto shule ya msingi tinde akiwasilisha taarifa ya utekelezaji.

Afisa Maendeleo kata ya tinde,Eva E.Mlowe akiwasilsha taarifa ya kata ya tinde.

Atupokile Maseta ,Afisa maendeleo ya jamii kata ya masengwa akiwasilisha taarifa ya kata ya masengwa.

Naomi Paul Afisa ustawi jamii halmshauri ya Shinyanga akiwasilisha taarifa yake kuhusu hali ya ukatili
Wadau kutoka kata ya tinde wakijadilia mipango wa kutokomeza ukatili kwa awamu ya pili


Wadau kutoka kaya ya masengwa wakijadili kuhusu hatua ya mipango kazi wa awamu ya pili wa mradi wa vunja ukimya,zuia ndoa na mimba za utotoni katika kata ya masengwa. Mipango ya utekelezaji ikiandaliwa kwa kata za tinde na masengwa.

Happyness Misael ,Msajili Msaidizi wa mashirika yasiyo ya serikali katika wilaya ya shinyanga

Joram Magana afisa maendeleo wa wilaya ya shinyanga azingumza mchango wa wadau katika wilaya hiyo.
Post a Comment

0 Comments