Header Ads Widget

WAZAZI WASIKWEPE MALEZI, SUNGUSUNGU & WAGANGA WAJITAFAKARI, ASASI ZA USHOGA HAZITAKIWI WILAYA YA SHINYANGA

 


Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Johari samizi akizungumza katika kongamano la mwaka la SHYEVAWC 







Wadau wa kupinga ukatili kutoka mkoa wa Shinyanga na mikoa mingine wakisikiliza mada mbalimbali za ukatili.

Na mwandishi wetu.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Johari Samizi ametoa kauli yake juu ya hali ya ulinzi na usalama dhidi ya vitendo vya ukatili katika wilaya ya shinyanga kwa kuagiza wazazi,sungusungu,waganga wa jadi na asasi za kiraia  na kujiepusha  na tabia ya kuendeleza vitendo vya ukatili katika jamii.

Hayo yameelezwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Bi.Johari Samizi katika Kongamano la umoja wa asasi za kirai zinazojihusisha na kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwa mkoa wa Shinyanga (Shinyanga EVAWC working Group)lilofanyika machi 9,2023 katika manispaa ya Shinyanga, ambapo asasi za kirai ishirini na nane na wadau wengine waliweza kushiriki kwa kujadili mada mbalimbali za kutokomeza kuweza  ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Shinyanga Ending violence against Women and Children working group(SHYEVAWC), waliitisha Kongamano hilo kwa ajili ya kufanya thathimi na wadau juu ya utekelezaji wa shughuli za mwaka 2022 katika kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.

Mwenyekiti wa Shyevawc working group, Jonathan Manyama amesema kuwa ni kundi la hiari kwa asasi za kiraia ishirini na nane za mkoa wa Shinyanga zinatokeleza miradi ya kutokomeza ukatili kwa mkoa wa Shinyanga.Ambapo limeundwa na maeneo manne ya uratibu,uthibiti,huduma na mawasiliano ambapo wanachama wa kuwekwa katika makundi hayo.

“Tumeunganisha nguvu zetu na kuweza kushirikishana ili kusaidia watoto na wanawake wa mkoa wetu,wazo lilianza na watu sita na leo tuko ishirini na nane kwa safari hii ya miaka miwili,Tuko hapa ili kujitathimini juu ya utekelezaji wa shughuli zetu ili kupokea mawazo ya wengine na kupata mbinu zingine”Amesema Jonathan

Watu wenye ubinfasi kufikiri wanaweza wakiwa pekee yao,ila pindi wanapojikuta hawawezi ndipo wanabaki wapweke,umoja wetu una maana zaidi na tunawakaribisha wale wote wasiotaka kukaa pekee yao kujiunga nasi”amesema Jonathan

Naye Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Johari Samizi alisema ni muhumu wazazi na walezi kuhakikisha wanalea watoto wao kwa maadili na kuwa makini na wasaidizi wa majumbani kwao na kuwapa uhuru ili wasiweze kutumia tamaa zao za kimwili kuharibu watoto na aliwataka wazazi kuelewa dhana ya serikali ya kutopeleka watoto wa umri mdogo wa  shule za kulala moja kwa moja.

“Hatupaswi kukwepa jukumu la kulea watoto,suala ya kuepeleka watoto wa umri wa miaka mitatu kwa shule za kulala moja kwa moja ni ukatili kwa watoto na hata kutowapa wasaidizi wa majumbani muda wao wa kupumzika ni ukatili pia”Amesema Johari

Aidha Johari alisema ,sungusungu ni vema wahakikishe wanatumia nguvu zao kuwafichua wabakaji na wanaowapa mimba watoto huko pembezoni kuliko kuweka adhabu na mihemuko kwa watu wazima wanaowafumaniwa katika maeneo yao.

Pia waganga wa jadi wanaotoa tiba mbadala,yamkini wapo ambao hawana nia njema na huduma za afya zaidi ya kuchochea ukatili dhidi ya wanawake na watoto ni lazima ifikie hatua ya kuwatambua vizuri.

“Kuna mitazamo wa sungusungu kuweka nguvu nyingi juu ya adhabu na kuwatafuta watu wazima wanaofumaniwa kuliko kuwafichua wabakaji na wale wanaowapa mimba watoto wa shule.” Amesema Johari.

Kwa upande mwingine,Johari alisema hataweza kuruhusu baadhi ya asasi za kiraia zinazo chochea masuala ya ushoga katika wilaya ya Shinyanga kwani ni kinyume na maadili yetu.

“Kwa wakati wangu ,sitakubali kuona asasi inayojihusha na kuchochea ushoga inafanya kazi katika wilaya hii,maana tunaharibu watoto wetu na hali imekuwa si nzuri kutokana na vitendo hivyo kuendelea kwa watoto wetu kila siku”Amesema Johari.

 

Post a Comment

0 Comments