Header Ads Widget

TGNP YAWASILISHA RASIMU YA SERA YA JINSIA CHAUMMA

 

Mwezeshaji kutoka TGNP, Bw.Deogratius Temba wakati akiwasilisha rasimu ya Sera ya Jinsia ya Chama cha CHAUMMA mbele ya Kamati Kuu ya Chama hicho leo Machi 11, 2023 katika ofisi za Chama hicho  Jijini Dar es Salaam.

Mwezeshaji kutoka TGNP, Bw.Deogratius Temba wakati akiwasilisha rasimu ya Sera ya Jinsia ya Chama cha CHAUMMA mbele ya Kamati Kuu ya Chama hicho leo Machi 11, 2023 katika ofisi za Chama hicho  Jijini Dar es Salaam.

*********************

NA EMMANUEL  MBATILO,  DAR ES SALAAM

KUTOKANA na Changamoto ya Ushiriki wa Wanawake, Vijana  na Watu wenye ulemavu kwenye siasa hasa kwenye nafasi za uongozi  na maamuzi ndani ya vyama vya siasa TGNP iliona  ni muhimu mkubwa kushirikiana  na Ofisi ya Msajili  wa Vyama vya Siasa kuviwezesha vyama kutengeneza sera ya jinsia, na moja ya Chama ambacho  kilinufaika kwa mara ya kwanza ni Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA).

Ameyasema hayo leo Machi 11,2023 Jijini  Dar es Salaam, Mwezeshaji kutoka TGNP, Bw.Deogratius Temba wakati akiwasilisha rasimu ya Sera ya Jinsia ya Chama cha CHAUMMA mbele ya Kamati Kuu ya Chama hicho ili baadae kiweze kupeleka rasmi hiyo katika Mkutano Mkuu wa Chama hicho.

Akiwasilisha rasimu hiyo Bw.Temba amesema rasmi ya Sera ya Jinisia kwa CHAUMMA inakwenda kusaidia  kukua kwa dhana ya demokraisia ya Kijamii kwa sababu wanawake, vijana, wazee na watu wenye ulemavu watapata fursa sawa ndani na nje ya chama hicho hasa katika masuala ya maamuzi.

Amesema katika mikakati  ya sera hiyo, inaenda kuboresha dhana ya “Ubwabwa wa maharagwe” ili kuwa na Jamii yenye ustawi kwa kuboresha huduma za jamii hasa afya, ustawi, elimu na maji safi na salama.

"Wakati  nawasilisha rasmi hii,  CHAUMMA wametoa mapendekezo machache ya  kuboresha lakini wameipenda kwani  inaonesha na kutafsiri vizuri  falsa yao ya Ubwawa na Maharage mashuleni". Amesema 

Pamoja  na hayo Bw.Temba amesema kuwa katika misingi ya Chama hicho, katika Katiba yake (2015), na  Kanuni za uendeshaji toleo la 2012,  kimebainisha misingi ya itikadi yake  kuwa  binadamu wote sawa, binadamu wanastahili kuwa huru na kulinda utu wao bila kukandamizwa na mtu yeyote kwa misingi  rangi,  kabila na jinsia.

Ameeleza kuwa dhumuni ya hii sera ni kuhakikisha wanawake wanashiriki  kikamilifu  kwenye nafasi za uongozi wa kisiasa na maamuzi  ili kuweza  kuonesha ujuzi wao katika uongozi licha ya baadhi  ya jamii  kuamini wanawake hawawezi katika uongozi na kufanya maamuzi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CHAUMMA Hashim Rungwe  amesema wamependezwa  na uwasilishwaji wa rasimu ya sera  ya Jinsia ya Chama hicho hivyo basi watahakikisha sera hiyo inatekelezwa ndani ya chama na wataanza kutafuta rasilimali  fedha kwaajili ya kutekeleza  sera hiyo.

Kamati Kuu ya Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) kikiongozwa na Mwenyekiti wao Hashim Rungwe wakimsikiliza Mwezeshaji kutoka TGNP, Bw.Deogratius Temba (hayupo  pichani) wakati akiwasilisha rasimu ya Sera ya Jinsia ya Chama cha CHAUMMA leo Machi 11, 2023 katika ofisi za Chama hicho  Jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) Hashim Rungwe akipendekez jambo mara baada ya Mwezeshaji kutoka TGNP, Bw.Deogratius Temba (hayupo  pichani) kuwasilisha rasimu ya Sera ya Jinsia ya Chama cha CHAUMMA leo Machi 11, 2023 katika ofisi za Chama hicho  Jijini Dar es Salaam.Kamati Kuu ya Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) kikiongozwa na Mwenyekiti wao Hashim Rungwe wakipata picha ya pamoja na Mwezeshaji kutoka TGNP, Bw.Deogratius Temba mara baada ya kumisikiliza akiwasilisha rasimu ya Sera ya Jinsia  ya chama hicho leo Machi 11, 2023 katika ofisi za CHAUMMA Jijini Dar es Salaam.Kamati Kuu ya Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) kikiongozwa na Mwenyekiti wao Hashim Rungwe wakipata picha ya pamoja baada ya kusikiliza uwasilishwaji wa rasimu ya Sera ya Jinsia ya Chama hicho kutoka kwa Mwezeshaji wa TGNP, Bw.Deogratius Temba mara baada ya kumisikiliza akiwasilisha rasimu ya Sera ya Jinsia  ya chama hicho leo Machi 11, 2023 katika ofisi za CHAUMMA Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL  MBATILO)

Post a Comment

0 Comments