Header Ads Widget

MATUKIO YA UKATILI MENGI YANAWATOKEA WANAWAKE JAMII YATAKIWA KUBADILIKA





 Wanawake wa kata ya Mwakata halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga wakisherekea siku ya wanawake duniani

Na  Kareny Masasy, Msalala

KATIBU  tawala wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga  Timothy Ndanya  amesema  matukio ya ukatili  sehemu kubwa yamewagusa wanawake  hivyo ameitaka jamii kubadilika kuacha vitendo vya ubakaji na ulawiti pamoja na vipigo.

Ndanya amesema hayo leo tarehe 07/03/2023  kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani alipokuwa mgeni rasmi katika halmashauri ya Msalala yaliyofanyika kwenye kata ya Mwakata .

“Nani siku hizi anapiga mwanamke ilikuwa zamani  siku hizi wanawake wanajishughulisha  nakujiunga vikundi  ikiwa halmashauri imekuwa ikitenga asilimia 4  mapato yake ya ndani  kwaajili ya kukopesha vikundi vya  wanawake vijana na watu wenye ulemavu”amesema Ndanya.

Katibu wa mpango mkakati  wa kutokomeza vitendo vya ukatili kutoka halmashauri ya Msalala  (MTAKUWWA)Veronica Mfuko amesema  siku ya wanawake imeanza kuazimishwa mwaka 1997.

Mfumko amesema ukatili wa kimwili  kwa watoto wakiume ni  96 na watoto wa kike  296 jumla yao  392 ikiwa ukatili wa kingono wanaume tisa na wasichana 15 jumla 22 ukatili wa kisaikolojia  wanaume 106 na wanawake 332 jumla 438 na ,ukatili wa kiuchumi wanaume sifuri na wanawake watano.

“Wafadhili kutoka UNFPA wamejenga kituo shufaa yaani one stop centre ambapo kipo kata ya Bugarama na dawati la jinsia kituo cha Polisi Bugarama”amesema Mfuko..

Mfuko amesema watoa huduma ngazi ya jamii wamejengewa uwezo wa  namna ya kuhudumia mtu aliyefanyiwa ukatili ambapo ipo changamoto ndugu kwa ndugu wanaofanyiana ukatili kumalizana kwa siri bila kuripoti masuala ya ukatili.

Ofisa maendeleo ya jamii  halmashauri ya Msalala  Judica Sumari amesema  wanawake  kutengewa siku hii lengo kupata fursa ya elimu namna ya kupambana na haki zao ambazo walikuwa wakizikosa  ambapo  wamekuwa wakifanya kazi kubwa nani tegemeo.

Sumari amesema wanawake ni walezi,walimu wa watoto  wanahitaji kupongezwa  ndiyo siku hii imepangwa ili kuelezana haki za msingi kwani walikuwa wanakosa kumiliki  ardhi na watoto wa kike kutopelekwa shule.

Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya Msalala  Flora Sagasaga amesema  bado jamii inaelewa baba ndiyo kiongozi wa familia  hilo ni sasa lakini dunia ya sasa imebadilika wanaume wameelimika nakutoa uhuru kwa wake zao.

“Zamani mwanamke alikuwa akiogopa kujiunga kikundi  kwa hofu ya kufokewa na mume wake sasa hakuna kilichobaki sisi wanawake tuwapende waume zetu na watoto ndani ya familia nakuepuka vitendo vya ukatili”amesema Sagasaga.


Wageni waalikwa wakiwa meza kuu  tayari kwa maadhimisho ya siku ya wanawake  yaliyofanyika kata ya Mwakata

Mgeni rasmi mkono wa kushoto ambaye ni katibu tawala wilaya ya Kahama Timothy Ndanya akiwa na diwani wa kata ya Mwakata Six Masanja

Wanafunzi wa shule ya sekondari Mwakata  wakijiandaa kuanza   kusherehesha

Baadhi ya watumishi wa halmashauri ya Msalala wakifuatilia  maadhimisho ya sherehe

Ofisa maendeleo wa halmashauri ya  Msalala  Judica Sumari akizungumza kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya wanawake

Mfanyakazi wa  shirika la KIWOHEDE  akipokea cheti  cha shukrani kutoka halmashauri ya Msalala

Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya  Msalala Flora  Sagasaga akiongea kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya wanawake

Diwani wa kata ya Mwakata Six Masanja akiongea kwenye sherehe za siku ya wanawake


Wananchi wa kata ya Mwakata wakifutilia matukio kwenye sherehe za siku ya wanawake

Post a Comment

0 Comments