Header Ads Widget

MAIPAC YASAMBAZA VITABU VYA MAARIFA YA ASILI UTUNZAJI WA MAZINGIRA NGORONGORO, WAZIRI JAFO AVIZINDUA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dr Seleman Jafo(kushoto) akizidua vitabu vya maarifa ya asili vya utunzaji wa mazingira (kulia) ni Mkurugenzi wa MAIPAC Mussa Juma.MAIPAC yasambaza vitabu vya maarifa ya asili katika utunzwaji Mazingira Ngorongoro.

Shirika la wanahabari la kusaidia jamii za Pembezoni (MAIPAC) limeanza kusambaza vitabu vya maarifa ya asili katika utunzaji wa Mazingira, misitu na Vyanzo vya maji, katika Wilaya ya Ngorongoro.

Vitabu hivyo,vilizinduliwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Dr Seleman Jafo jijini Arusha na kuagiza visambaze kwa wadau Ili kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi nchi.

Akizungumza wakati wa kugawa vitabu hivyo Kata ya Enguserosambu tarafa yaLoliondo wilaya ya Ngorongoro,Katibu wa Bodi ya Msitu wa jamii wa Enguserosambu,Mark Tarash amewataka wakazi wa Ngorongoro kuvitumia vitabu hivyo ni vizuri.

Tarish amesema kuwa Wakazi wa Kata ya Enguserosambu walishiriki katika kutoa simulizi za maarifa ya asili hivyo ni sehemu ya waliofanikisha kitabu hicho.

"MAIPAC walifika kijijini na kukaa na viongozi wa Mila,wazee, wajumbe wa Serikali za vijiji,walimu na Wanafunzi kukusanya taarifa hizi na Leo tumeona kitabu kimetoka"amesema

Amesema hata katika uhakiki wa kitabu MAIPAC iliwaalika jijini Arusha pamoja na viongozi wa Halmashauri ya Ngorongoro,Monduli na Longido kuhakiki taarifa zote kabla ya kuchapishwa vitabu.

Vitabu hivyo, ni sehemu ya mradi wa Uhifadhi na utunzwaji Mazingira kwa maarifa ya asili unaofadhiliwa na mfuko wa Mazingira duniani (GEF) kupitia shirika la maendeleo la umoja wa mataifa (UNDP) katika program ya miradi midogo.

Vitabu 3000 vinasambazwa katika wilaya za Longido,Monduli na Longido lakini pia katika taasisi mbalimbali za serikali na binafsi ndani na nje ya nchi.

Akizindua vitabu hivyo, wakati wa uzinduzi,Waziri Dk Jafu alisema vitakuwa na Msaada mkubwa kwani jamii kwa Sasa imeanza kusahau maarifa ya asili katika. mambo mbalimbali ya kijamii ikiwepo utunzwaji wa Mazingira.

Dk Jafo alisema kitabu hicho,kitapelekwa kwa wataalam wengine Ili kuona kinaweza kutumika zaidi katika eneo lipi.

Hata hivyo, Waziri  Dk Jafo alipongeza mfuko wa Mazingira dunian ( GEF) na UNDP kusaidia mashirika madogo kama MAIPAC katika miradi ya utunzaji Mazingira ambayo Inaguza  Moja Kwa Moja Wananchi.

"Nawaomba UNDP na GEF kuendelea kusaidia MAIPAC na wengine katika miradi hii kwani hali ya uhalibufu Mazingira ni mbaya Dunia na jitihada kubwa zinahitajika kwa kushirikiana wadau mbalimbali "alisema

Mratibu wa program  ya midogo ya Mazingira kupitia GEF ambayo inasimamiwa  na shirika la UNDP , Faustine Ninga alisema vitabu hivyo vitasaidia kurithisha maarifa ya asili kutoka vizazi vya Sasa na vijavyo.

Mkurugenzi wa MAIPAC,Mussa Juma  alisema shirika la MAIPAC wa kushirikiana na shirika la CILAO pia wametengeneza makala ndefu na fupi za video za maarifa ya asili ambazo zitaendea kusambaza kwenye vyombo vya habari .

"Vitabu hivi tunatarajia vitasomwa na Wanafunzi,vijana , wanawake na makundi mengine katika jamii ikiwepo watungaji wa sera Ili kusaidia kutunzwa Mazingira "amesema

Afisa Maendeleo ya Jamii mkoa Arusha,Blandina Nkini alipongeza pia MAIPAC kuwa na mradi wa kipekee wa Uhifadhi Mazingira kwa maarifa ya asili na kueleza anajivunia shirika hilo pekee kati ya mashirika 1114 mkoa Arusha linalofanya kazi nzuri ya kuhimiza utunzwaji Mazingira kwa maarifa ya asili.

"Mimi najivunia Sana uwepo wa shirika hili la wanahabari  la MAIPAC hapa mkoani Arusha kwani limekuwa na ushirikiano mzuri na Serikali na hususani Ofisi yangu katika utekelezaji wa miradi na natoa wito mashirika mengine kuiga"amesema.


Post a Comment

0 Comments