Header Ads Widget

NAIBU WAZIRI AIPONGEZA DON BOSCO KWA KUHAMASISHA MICHEZO SHULENI AZITAKA, HALMASHAURI NCHINI KUWA NA VIWANJA VYA MICHEZONaibu Waziri Utamaduni,Sanaa na Michezo Pauline Gekul akizungumza kwenye tamasha la michezo shule ya sekondari Don Bosco 

              Naibu Waziri Utamaduni,Sanaa na Michezo Pauline Gekul akiwa na viongozi wengine wakielekea eneo la uwanja wa michezo shule ya sekondari Don Bosco
 
                              Na Shinyanga Press Club Blog

Naibu Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo Pauline Gekul amewataka maafisa michezo na maafisa utamaduni kuanzia ngazi ya Wilaya kuhakikisha wanazitembelea shule za msingi na sekondari ili kuona kama wanapata muda wa kushiriki kwenye michezo ili kuimarisha afya na kujiepusha na magonjwa.

 Naibu Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo Pauline Gekul ametoa agizo hilo February 18 alipotembelea shule ya sekondari Don Bosco Kata ya Didia Halmashauri ya Shinyanga na kushiriki tamasha la michezo lililoandaliwa na shule hiyo ambalo hufanyika kila mwaka.

Naibu Waziri Gekul ameipongeza shule ya Don Bosco kwa kuwa na utaratibu wa kuandaa matamasha ya michezo ambayo yanasaidia kuimarisha afya kwa walimu na wanafunzi na kuwawezesha kusoma vizuri bila kusumbuliwa na magonjwa.

“Nimefurahi sana kuona wanafunzi wanacheza michezo mbalimbali hii inaonesha wazi hata afya zao ziko vizuri,pia nimefurahi kuona mna kiwanja kizuri kwa ajili ya michezo,sasa natumia fursa hii kutoa maagizo kwa Halmashauri zote nchini ambazo hazina viwanja kutenga maeneo ya viwanja vya michezo” amesema, Gekul.

Naibu Waziri amewataka maafisa michezo na maafisa utamaduni kuhakikisha wanakagua viwanja vya michezo kama vina miundombinu inayotakiwa ili kuwawezesha watumiaji kufanya mazoezi bila kuwa na changamoto.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri amewataka wanafunzi kujiepusha na makundi ambayo yanaweza kuharibu ndoto zao kutokana na kwamba maadili yameporomoka katika jamii huku akisisitiza suala la kuwa na hofu ya Mungu na kuzingatia kilichowapeleka shule kupata elimu ili kutimiza malengo yao.

 "Pamoja na kuhamasisha michezo lakini mimi kama mama yenu ni lazima nitoe nasaha kama mzazi,maana suala la maadili limekuwa ni tatizo kubwa wapo mabinti wanakatisha ndoto zao kwa kupata ujauzito na kukatisha ndoto zao amsijiingize kwenye mahusiano zingatieni masomo'' amesema Naibu Waziri.

Mwalimu wa michezo shule ya Sekondari Don Bosco Zipapa James amesema michezo imesaidia kujenga undugu na urafiki pamoja na kuimarisha afya kwa wanafunzi na walimu na kuwawezesha kufanya vizuri kwenye masomo yao.      Mmoja wa wanafunzi wa shule ya Sekondari Don Bosco Kata ya Didia akimvisha skafu Naibu Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Pauline Gekul  baada ya kuwasili katika shule hiyo.

                   Mkuu wa shule ya Sekondari Don Bosco Felix Wagi akizungumza wakati wa tamasha la michezo


                                     
Diwani wa Kata ya Didia Richard Luhende
Naibu Waziri Utamaduni sanaa na michezo Pauline Gekuli akikagua kazi zilizoandaliwa na wanafunzi


                              Wanafunzi wa shule ya sekondari Don Bosco
                Wanafunzi wakionesha michezo mbalimbali
 

Post a Comment

0 Comments