Header Ads Widget

MRADI WA VYOMBO VYA HABARI SHINYANGA, WALETA MATOKEO YA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI NA KUEPUSHA WANAFUNZI KUTEMBEA UMBALI MREFU.

 

MRADI WA VYOMBO VYA HABARI SHINYANGA, WALETA MATOKEO YA UJENZI WA SHULE YA SEKONDARI NA KUEPUSHA WANAFUNZI KUTEMBEA UMBALI MREFU.

                                         


Majengo ya madarasa ya shule ya sekondari ya luhumbo iliyoka kata ya didia.



Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa mwaka 2023 waliopokelewa katika shule ya sekondari luhumbo.








Wanafunzi wakiwa darasani wakiendelea na masomo katika shule ya sekondari Luhumbo.
Diwani wa kata ya Didia ,Luhende Masele akiongea na vyombo vya habari kuhusu matokeo ya ujenzi wa shule kwa nguvu za serikali na wananchi.
Na mwandishi wetu

Serikali na wananchi wa kata ya didia wafanikiwa kuanzisha shule ya sekondari Luhumbo kwa ajili ya kunusuru watoto wanaotembea umbali mrefu zaidi ya kilomita nane(8) kila siku baada ya juhudi za pamoja zilizoanza toka mwezi machi,2021 baada ya vyombo vya habari kupaza sauti ya uwepo wa matukio ya ukatili unaosababishwa na wanafunzi kutembea na umbali mrefu.

Ukamilishaji wa shule ya sekondari Luhumbo katika kata ya didia umetokana na Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Shinyanga kupaza sauti kupitia mradi wa “Nafasi ya vyombo vya habari katika kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto” uliotekeleza kwa kipindi cha januari hadi machi,2021 na kwa ufadhili wa Mfuko wa wanawake Tanzania (Women Fund Tanzania) katika Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga imefanya ufatiliaji wa matokeo ya mradi huo februari,2023 na kubaini jamii na serikali kufanikiwa kujenga madarasa manne na matundu kumi na mbili ya vyoo kwa jumla ya Tshs million 95 ambapo serikali imegharamia kwa Tshs million 80 na wananchi kwa Tshs milioni15.

Shule ya sekondari luhumbo imefanikiwa kupokea wanafunzi 135(ME-74, KE-61) kwa mwaka 2023 na kusaidia wanafunzi kuepuka umbali wa kilomita 8 kwenda hadi shule ya sekondari didia.Hayo yameelezwa na diwani wa kata ya Didia ,Bwana Luhende Masele wakati akiongea na vyombo vya habari,Februari 8,2023.

Diwani wa kata ya didia, Luhende Masele alisema,Tumefanikiwa kupunguza utoro na kuokoa watoto kutembea umbali mrefu zaidi ya kilomita 8 na kuwaepusha na matukio kadhaa ya vitendo vya ukatili ikiwa ni kubakwa,mimba za utotoni na hata kutishiwa na wanyama wakali wakati wa jioni na asubuhi.

Masele alisema,Tumefanikiwa kwa hatua za awali kuwa na sekondari hii kwa eneo letu na tumebaki na changamoto ya maabara na ofisi ya waalimu na tunayo mipango ya kuweka juhudi za pamoja tena ili kuweza kukamilisha na hata kuweka ukuta kwa ajili ya usalama na ulinzi wa wanafunzi.

“Wadau wa ukatili kwa kushirikiana na vyombo vya habari waliweza kuibua habari matokeo katika dhamira ya kupinga ukatili kwa kupaza sauti.Jamii ilipokea mrejesho baada ya sauti ya vyombo vya habari na ikaweka mipango ya kutenga eneo la hekari 10 ili kuweza Kujenga shule ili kusaidia wanafunzi”Alisema Masele.

“Mimi kama kiongozi wa kata,nilipokea mrejesho na kuweza  kutumia jukwaa la baraza la madiwani la Halmashauri kuweza kupeleka hoja ya wananchi na kushawishi serikali kuweza kutupatia rasilImali fedha ili kuweza kukamilisha ujenzi wa shule hii na ambapo serikali iliridhia na kutupatia kiasi cha Tshs million 80  na kutupa jukumu la jamii kukamilisha miundio mbinu ya matundu ya vyoo vya shule,Jamii ilishiriki kwa nguvu zao na michango ya fedha kwa kiasi cha Tshs million 15” Alisema Masele.

Aidha Afisa Elimu wa Kata,Justus C.Birago, Alisema tulijadili suala hili kupitia vikao vya kata na tumefanikwa kupata shule ya wanafunzi 135 kwa mwaka huu kutoka katika kata na kusaidia watoto kutotembea kilomita 8 hadi shule ya sekondari didia iliyoko kijiji cha bukumbi.Jamii iliweza kutenga eneo la ekari 10 kwa manufaa ya watoto wao.

“Tunashukuru serikali na wadau kwa hatua za awali za kuleta matokeo katika elimu kwa kata hii na vema basi tuwe pamoja katika ukamilishaji wa chumba cha waalimu na maabara.Tumeshuhudia nguvu vya vyombo vya habari katika utekelezaji wa mradi wao kwa matokeo ya shule hii kuwepo na kutoa huduma”Alisema Birago

“Kupitia vikao vya ODC,tuliomba serikali kuelekeza fedha za UVIKO zitumike kujenga madarasa manne ya shule katika eneo letu kutokana na changamoto iliyopo na walikubali na walituagiza tuishirikishe jamii kukamilisha sehemu ya matundu ya vyoo na chumba cha maabara”Alisema Birago

Kwa upande wake, Juma L.Kisenha,Makamu wa shule hiyo,Alisema hadi leo februari 8,2023 wanafunzi walipokelewa ni 136 kwa wanaotoka ndani ya kata hiyo na anashukuru serikali kwa sehemu kubwa ya kuweka nguvu ya ujenzi wa madarasa hayo.

Baadhi ya wanafunzi walioongea na vyombo vya habari, walidai imesadia wao kutotembea umbali mrefu na kuwaepusha na vitendo vya ukatili.

“shule imetusaidia kutotembea umbali mrefu na hasa wasicha watakwepa vishawishi kutoka kwa makundi ya mitaani ya vijana.” Alisema Petro Masunga (18)

“Naishukuru serikali kwa kutujengea shule hii na itatusaidia kutotembea umbali mrefu wa kwenda kule shule ya sekondari didia”Alisema Magreth Robert(13)

“Hii itatusaida hata kupanda kitaalum na kuwa hatutaweza kuchoka sana kwa kutembea umbali mrefu zaidi” Alisema Erick Salu shija(16)

Magesa Faustine mkazi wa kata ya didia ,alisema vyombo vya habari vimeleta matokeo ya uwepo makubwa ya kuweza kutatua changamoto ya watoto wetu kutembwa umbali mrefu.

 



Wanafunzi wa shule ya sekondari luhumbo wakiongea na vyombo vya habari.

 

Matundu ya vyoo vya wavulana
Matundu ya vyoo kwa wasichana.


Matundu ya vyoo kwa ajili ya waalimu .

Post a Comment

0 Comments