Header Ads Widget

WAZAZI WACHANGAMKA UANDIKISHAJI WA DARASA LA AWALI


 Moja ya wanafunzi wa darasa la awali wakiwa kwenye hali ya ujifunzaji.

Na  Kareny  Masasy

Tanzania ni nchi ya kwanza katika ukanda wa Afrika Mashariki  katika elimu ya awali kuifanya kuwa ya lazima kwenye sera ya elimu na mafunzo  ya mwaka 2014.

Ilijumuisha  elimu ya awali  katika  elimu ya msingi  kwa kuzingatia  shule zote  kuwa na darasa la elimu ya awali  kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano.

Aidha uandikishwaji  wa elimu ya awali  nikiashiria  muhimu  kilichongizwa  katika mpango  wa taifa  wa maendeleo  ya miaka mitano  2016/17-2020/21.

 Saada Robert  mkazi wa kitongoji cha Mwashagi kijiji cha Lyabukande  halmashauri ya wilaya ya Shinyanga mwenye watoto wawili mmoja anamiaka nane na mwingine miaka 6 amejitokeza kuandikisha watoto hao.

“Nimekuja kuwaandikisha wanangu  waanze darasa la awali  walichukuliwa  na baba yao na kuwatelekeza nyumbani kwao kijijini”anasema Robert.

Robert anasema amewafuata mkoani Tabora    baada ya kusikia hawasomi  wanachunga mifugo ya bibi yao.

“Nilikasirika sana kusikia wanangu hawasomi na baba yao kakalia ulevi tu…….”anasema Robert.

Sofia Charles Mkazi wa kijiji cha Lyabukande anasema  ameona umri wa mtoto wake  mwenye miaka mitano unatosha kuanza darasa la awali  kama wanavyoelezwa na serikali aanze  darasa la awali kwanza.

“Nimemleta bila sare za shule nikipata pesa baadaye nitamnunulia ngoja kwanza aendelee kujifunza”anasema Charles.

Pendo Mayala anasema amekuja kumuandikisha mtoto wake mwenye umri wa miaka nane  kuanza darasa la awali sababu alikuwa akiishi na babu yake kijiji jirani.

Mwenyekiti wa kijiji cha Lyabukande  Peter  Labacha anasema  wameweka mpango mkakati wa kuhakikisha kila mzazi  mwenye mtoto anayetakiwa kuanza shule aanze.

“Baadhi  ya wazazi  wameanza kuelewa  wanawapeleka shule  watoto na majira ya saa tano  wanapotoka  huwafuata hadi shuleni”anasema Labacha.

Mwalimu  Nyebu Musa anayefundisha darasa la awali shule ya msingi Lyabukande anasema wazazi wamepata mwamko wa kuleta watoto.

“Zipo mbinu za ufundishaji wa watoto ili waendelee kuipenda  hawa ukiwakemea kesho darasa zima hawaji shule “anasema Mwalimu Musa.

Musa anasema mara nyingi wamekuwa wakiimba nyimbo,kucheza na kusimulia hadithi  ambayo wataifurahia.

Musa anasema darasa moja lina wanafunzi  42 walioandikishwa mpaka sasa wasichana ni 22 na wavulana ni 20 hivyo takwimu hii inaenda ikiongezeka kila siku za shule wanaripoti.

Musa anasema mwaka jana walikuwa wanafunzi 150 darasa moja  wakianzia umri wa miaka minne hadi  nane.

‘Mwanafunzi akionekana umri wake ni mkubwa hawamuweki  darasa la awali  anavukishwa kwenda darasa la kwanza kwa matazamio ya kujua KKK”anasema Musa.

Musa anasema wanaishukuru  serikali kuhimiza watoto walio na umri wa miaka minne waanze shule baadhi wenye miaka mitano wameingia darasa la kwanza wakijua KKK.

Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Lyabukande  Jeremiah Mashaka anasema shule hiyo ilianzishwa mwaka 1956  walikuwa hawana mwalimu wakufundisha darasa la awali.

Mwalimu Mshaka anasema baada ya sera kuelezwa kila shule iwe na darasa la awali ikalazimika kutafuta mwalimu  mwaka jana aliyepitia  mafunzo na kujitolea.

Mratibu elimu kata ya Kyabukande  Harun Ibrahimu anasema kata yake ina vijiji saba na kila kijiji kina  shule  ya msingi lenye darasa la awali.

Ibrahimu anasema uandikishwaji wa watoto  huwa wanautangaza kwenye mkutano wa hadhara ili kila mzazi mwenye mtoto wa umri wa kuanza shule andikishwe.

Ofisa elimu msingi kutoka halmashauri ya wilaya ya Shinyanga  Christina Bukori anasema matarajio ya uandikishaji wa darasa la awali ni watoto 11,136 na walioandikishwa mpaka sasa ni watoto 10,122 sawa na asilimia 96.

Bukori  anasema wazazi wamepata mwamko wa kuandikisha watoto shule kwa mwaka jana waliandikishwa watoto zaidi ya 10,000.

Ofisa elimu mkoa wa Shinyanga Dafrosa Ndalichako  anasema  madarasa ya awali ni 672  kutokana sera ya elimu na mafunzo ya mwaka 2014 inaeleza kila shule ya msingi kuwe na darasa la awali.

Elimu ya awali wanafunzi  waliondikishwa mpaka sasa mwaka 2023  ni   45287 sawa na asilimia 97.1 ambapo halmashauri ya wilaya ya Shinyanga ina asilimia 96 katika uandikishaji huo.

uandikishaji huo  kipindi cha mwaka 2021   mkoa wa Shinyanga  uliandikisha watoto wa kuanzia  miaka mitatu  hadi  zaidi ya miaka mitano  watoto  42552  .

Mshauri  wa malezi,makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto  kutoka shirika la  Children in Crossfire (CiC)  Davis Gisuka anasema mtoto anapopata elimu ya awali inamjengea uchangamfu na uelewa wa vitu mbalimbali kwake.

“Kuna faida mtoto kuanza darasa la awali maana darasa la awali zaidi atajifunza nyimbo zenye ujumbe,michezo na hadithi  na mbinu hiyo itamfanya kuweka kumbukumu na   kujua kuhesabu namba”anasema Gisuka..

Waziri wa nchi  ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa  (TAMISEMI) Angela Kairuki  amesema mchakato wa uandikishaji wa darasa la awali uendelee.

“Ninasema watoto wenye umri wa miaka minne hadi mitano waanze darasa la awali ili wawe na ufahamu mzuri darasani na kuondoa wanafunzi wasio jua KKK”anasema  Kairuki.

Kwa mujibu wa programu jumuishi ya Taifa ya malezi,makuzi  na maendeleo ya awali ya mtoto  PJT-MMMAM 2021/22-2025/26 inaeleza  kuwepo mazingira  rafiki  ya kisera kumepelekea  ongezeko la uandikishwaji wa watoto.

Ndani ya mwaka mmoja umefikia uandikishaji 500,000 kutoka 1,069 823 mwaka 2015  mpaka 1,562,770 mwaka 2016.

Ilani ya  Uchaguzi ya chama cha Mapinduzi  (CCM)imeeleza  Kuongezeka kwa uandikishaji  wa wanafunzi wa elimu ya  awali kutoka 1,069,823 mwaka 2015  hadi kufikia 1,429,169 mwaka 2020.


 

 

Post a Comment

0 Comments