Header Ads Widget

RAIS SAMIA AFANYA MABADILIKO YA VIONGOZI SERIKALINI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko ya nafasi za uongozi katika Serikali ambapo amemteua Balozi Hussein Othman Katanga kuwa Balozi wa Tanzania mjini New York, nchini Marekani na Mwakilishi wa Kudumu katika Umoja wa Mataifa.


Kupitia taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais Ikulu Zuhura Yunus leo Jumanne Januari 03, 2022 imeeleza kuwa Balozi Katanga amechukua nafasi ya Balozi Profesa Kennedy Gaston ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Kabla ya uteuzi huu balozi Katanga alikuwa Katibu Mkuu Kiongozi.

Rais Samia amemteua Bw. Moses Mpogole Kusiluka kuwa Katibu Mkuu Kiongozi ambapo Kabla ya Uteuzi huo Bw. Kusiluka alikuwa Katibu Mkuu Ikulu

Kamishna Diwani Athumani Msuya ameteulwa kuwa Katibu Mkuu Ikulu ambapo Kabla ya uteuzi huo Kamishna Diwani alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Pia Rais Samia amemteua Bw. Said Hussein Masoro kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa ambapo Kabla ya uteuzi huo Bw. Masoro alikuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu na Mkurugenzi wa Shughuli za Ndani wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa uteuzi huu unaanza mara moja.


Post a Comment

0 Comments