Header Ads Widget

JUMUIYA CHOMBO CHA WATUMIA MAJI SHINYANGA WAIFURAHISHA RUWASA KATIKA UTENDAJI WAO.
Mkurugenzi mkuu wa Ruwasa Mhandisi  Clement Kivegalo akitoa maelezo kwa  meneja wa Ruwasa wilaya ya Shinyanga  Mhandisi  Emael Nkopi  na mtekelezaji wa mradi  kutoka kampuni ya Healem Elias  Slyvester eneo la mradi wa maji.

Na  Kareny  Masasy,Shinyanga

MKURUGENZI  mkuu wa wakala wa maji na usafi wa mazingira vijijini (Ruwasa)  Mhandis  Clement Kivegalo amefurahishwa  na  jumuiya za chombo cha watumiaji maji (CBWSO) mkoani Shinyanga kwa ukusanyaji wa mapato na kufanyiwa ukaguzi.

Mhandis Kivegalo ameyasema hayo leo  tarehe 14/1/2023   alipohitimisha ziara yake mkoani hapa  ya ukaguaji wa miradi pamoja nakukutana na jumuiya za vijiji vya Ng’washi  kata ya Pandagishiza na  kijiji cha Songambele kata ya Salawe..

Mhandis Kivegalo amesema  jumuiya za watumia maji  zimeanza kupata uelewa tofauti na zamani   ambapo serikali ndiyo inavyotaka wajitegemee.

 Mhandis Kivegalo amesema amefurahishwa na jumuiya za watumiaji maji  kijiji cha Songambele wilaya ya Shinyanga kila mwezi makusanyo  zaidi ya  Millioni 19 na jumuiya ya Pasamwash ya kijiji cha Songambele    sh Millioni 4.

“Jumuiya hizi wanapokabidhiwa wanatakiwa kuhakikisha  wanatengeneza vituo vya kutolea maji  pamoja na kutoa elimu kwa wananchi  ”amesema  Kivegalo.

Meneja wa  Ruwasa wilaya ya Shinyanga  Mhandis Emael Nkopi amesema  miradi inayoendelea mojawapo ni wa kijiji cha Mawemilu  uliopo kata ya Mwakitolyo umekamilika kwa asilimia 95 gharama yake  sh Billioni 3 utanufaisha  wakazi 23,000.

Mwenyekiti wa jumuiya ya  chombo cha watumia maji kijiji cha Songambele  Monica Francis amesema mradi huo umewanufaisha wananchi nakupata kujiunga kwa wingi baada ya kuhamasishwa .

Mtendaji wa jumuiya  hiyo  Chagu Manyiluzi akisoma taarifa mbele ya mkurugenzi huyo amesema  mradi  unahudumia vijiji 10 kwa watu  45,116 chanzo chake ni bomba la maji ziwa victori

Diwani wa kata ya Salawe Joseph Buyugu amesema  wananchi wanapata huduma ya maji mita 200  kwani walikuwa wakifuata umbali wa kilomita 20 nakufikia hatua ya kubakwa.

ww
Tanki la maji lililojengwa kijiji cha Mawemilu kata ya Mwakitolyo

Mkandarsi wa kampuni ya Halem  Elias Slyvester  anayetekeleza mardi wa maji kijiji cha Mawemilu kata ya Mwakitolyo akizungumza na mkurugenzi mkuu wa Ruwasa   Mhandisi Kivegalo 

Ukaguzi wa tanki  la maji ukiendelea ambao  mradi umekamilika kwa asilimia 95Watumishi wa Ruwasa wakifuatilia  taarifa ya jumuiya ya chombo cha watumia maji kijiji cha SongameleMwenyekiti wa jumuiya ya chombo cha watumiaji maji Monica Francis akimsikiliza mkurugenzi mkuu Ruwasa Mhandis Kivegalo.

Meneja wa Ruwasa mkoa wa Shinyanga  aliyesimama Mhandisi Julieth Payovera  akitoa utambulisho kwenye kikao.
Mwenyekiti wa  jumuiya ya chombo cha watumia maji  kijiji cha Ng'washi kata ya Pandagichiza Magreth Magina akizungumza kwenye kikao.

Post a Comment

0 Comments