Header Ads Widget

HALMASHAURI YA MSALALA WILAYANI KAHAMA WAMEPATA CHANJO YA UVIKO -19 KWA HIARIAfisa mradi kutoka shirika la SHDEPHA+ Erick Mlimba akielezea utekelezaji wa mradi wa Uviko-19.

Na Kareny  Masasy,Kahama

WAKAZI  197,982  wa halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga wamepata  chanjo ya Uviko-19 kwa hiari  kuanzia mwaka 2021 hadi  tarehe 15, mwezi Januari,2023.

John Maongezi  ambaye ni afisa mradi  kutoka shirika la AMERICARE  lenye makazi yake  nchini Marekani ameongea  na waandishi wa  habari leo tarehe 17/01/20 23 mjini Kahama.

Maongezi amesema wao  wamelifadhili shirika la SHDEPHA+ lenye makazi yake wilayani Kahama  kwaajili ya  kuendeleza kutoa elimu kwenye jamii juu ya Uviko-19 na wamekuwa wakifanya kazi pamoja na wizara ya afya.

Kwa mkoa wa Shinyanga  tumeanza kazi  rasmi mwezi wa kumi mwaka 2022 katika halmashauri ya Msalala,Kishapu na Manispaa ya Shinyanga  kuhakikisha wanasogea karibu kutoa  huduma na kuhamasisha uchomaji wa chanjo.

Katika juhudi za kukwamua  mlipuko wa  Uviko-19 serikali  ya Tanzania mwaka 2021 ilikubali maekezo ya  shirika la afya duniani (WHO) kuhusu uchanjaji wa chanjo na wadau kuendeleza suala hilo.

“Walengwa waliotakiwa  kuchanjwa ni 164,259  na kila halmashauri ilipewa lengo lake na Msalala imevuka lengo nakufikia asilimia 102.2”amesema Maongezi.

Ameongeza “Tumefikia lengo lakini uchanjaji bado unaendelea kwani watu wa kuchanja wanahitajika sababu wapo wenye umri wa miaka 18 wamefikisha wanahitaji kuchanja”

Maongezi amesema baadhi ya watu walizungumza kwa kupotosha kuwa ukichanja damu itaganda hawata zaa,  watakuwa mazombi lakini waliochanja wako vizuri na wajawazito wanazaa na hakuna mtu aliyekuwa zombi wala kuganda damu” amesema

Afisa Mradi kutoka SHDEPHA+ Erick  Mlimba  amesema malengo ya mradi ni kuongeza uchanjaji wa chanjo katika njia tofauti tofauti ikiwa njia mojawapo kusambaza elimu sahihi nakufanya majadiliano na watu ambao wamekuwa na wasiwasi kuanzia ngazi ya vitongoji  hadi mkoa  pamoja na  Kuunganisha jamii na  watoa huduma. 

Kaimu  mganga mkuu wa halmashauri ya Msalala  wilayani Kahama mkoani Shinyanga  Peter  Shimbe ambaye ni muelimishaji wa masuala ya afya  anasema Covid-19 bado ipo  na watu waendelee kujikinga kwa kuchanja. 

Mratibu wa chanjo  halmashauri ya Msalala Basil Kafunja  anasema  watu walikuwa na mtazamo hasi  nakupotosha kuhusu chanjo ya uviko-19  kwa sasa wameelimika  na wamekuwa wakijitokeza kwa hiari kuchanja.

 “Serikali imeenda mbali zaidi kwa kutumia mbinu ya wauguzi kutembea kwenye kila nyumba  kuwafikia walengwa ambapo kuanzia mwezi Juni mwaka 2021 hadi Januari 15,2023 wamefanikiwa  kuwachanja watu 197,982 sawa na asilimia 102.2”amesema Kafunja. .


Afisa mradi   wa kuhamasisha  uchanjaji na watoa huduma kwa jamii  Erick Mlimba akiwa na mtathimini na mfatiliaji  Elizaberth  Laurent. kutoka shirika la SHDEPHA+

Afisa mradi kutoka shirika la Americare   John Maongezi


kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya Msalala  Peter Shimbe  akiwa na mratibu wa chanji Basil Kafunja wakisikiliza utekelezaji wa mradi 

Post a Comment

0 Comments