Header Ads Widget

HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI YAANZA KUTOA HUDUMA KUPUNGUZA UZITO


Muhimbili waanza kutoa huduma kupunguza uzito
Na Aveline KitomaryDecember 21, 2022
Muhimbili waanza kutoa huduma kupunza uzito

HOSPITALI ya Taifa ya Muhimbili-Mloganzila,iliyopo jijini Dar es Salaam, imeanza kutoa huduma ya kupunguza uzito uliokithiri, ikiwa ni hatua ya kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza.

Hadi sasa watu watatu wenye uzito zaidi ya kilogramu 100 wamepata huduma hiyo inayogharimu kiasi cha Sh milioni 3.5 hadi Sh milioni 4.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Prof Mohammed Janabi, alisema hawatoi huduma hiyo kwa sababu ya urembo bali wanalenga kusaidia watu.

“Hii ni operesheni yetu ya tatu leo na siku ya leo tumewafanyia watu wawili hawa wote ni kilo 100 kwenda juu, wa kwanza kilo 160 na wengine kilo 105, hawajafanya kwa sababu ya urembo.

“Wiki moja iliyopita tulifungua kliniki ya mafuta tunawakaribisha hospitali zingine ziweze kuleta wagonjwa wake kupata huduma,”amesisitiza Prof Janabi.

Amesema utoaji huduma hiyo utahusisha tumboni kupitia mdomo hali itakayopunguza kiwango cha chakula kwa muhusuka.

“Tutaweka kwa miezi nane, tutaingiza kupitia mdomo hadi kwenye tumbo hakuna upasuaji tutatumia mitambo ifike mahali pake tutajaza dawa linapunguza ukubwa wa tumbo ukila kidogo utashiba hivyo tunategemea uzito utapungua.

Prof Janabi ameeleza kuwa faida kubwa ni kusaidia kukukinga na magonjwa ya kisukari, kiharusi, moyo, kushindwa kupumua.

Amebainisha kuwa matibabu yatakayotolewa ni siri ya mgonjwa, ambapo pia matibabu hayo huchuku siku mbili tu.

“Siku ya kwanza unaweza kusikia kama unavidonda vya tumbo, lakini baada ya muda utaendelea kawaida, hospitali hatukaribishi watu lakini tunawaomba wale wenye uzito mkubwa wafike kliniki, tuna kliniki ya siku mbili hapa Mloganzila na siku mbili Muhimbili Upanga,” amesisitiza.

Pamoja na hayo amesema pindi mgonjwa anapopatiwa huduma hiyo na kupungua atapata usaidizi wa mtaalamu wa lishe, ili asiongeze tena kiwango cha kula na uzito kuongezeka tena.

“Kabla ya kumuhudumia tutapima vitu vingine vyote ndo utakuja kupata huduma, faida kubwa ni kitu ambacho baada ya miezi nane tutatoa na hali ya kula kidogo itaendelea na akirudi tabia ya mwanzo anaweza kuwekewa mara nyingine hivyo ni vyema kuweka kiasi,” amesema.

Amesema mfumo wa Bima ya afya bado haujaanza kutumika hata hivyo watu wafanye mazoezi, wale mlo unaotakiwa.

“Na matatizo mengine ni ya kurithi ukiwa na mtoto ana uzito mkubwa mleteni wakati mwingine unaweza kukuta mtoto amezaliwa na kilo nne watu wakaona ni kitu sahihi kumbe sio kweli,” amesema.

Amesema gharama ya huduma hiyo kwa India ni Sh milioni 15 hadi Sh milioni 20 na Ulaya ni kuanzia Sh milioni 30 kwenda juu.

Amesema mwaka 2023 kwa kipindi cha Januari wanatarajia kuwahudumia wagonjwa 12 kwa gharama ya Sh milioni 3.5 hadi Sh milioni 4.

“Hii ni sehemu ya utalii tiba, hivyo nchi za jirani tunatoa huduma hizi waje kupata huduma ni tiba salama kama tunavyopandikiza figo, uloto na zingine wakitaka kupata huduma hapa ni rahisi,”ameeleza Prof Janabi.

Chanzo: Habari Leo

Post a Comment

0 Comments