Header Ads Widget

WANANCHI MASENGWA WAADHIMISHA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA KWA KUPANDA MITI ILI KUFIKISHA UJUMBE WA KUMLINDA MTOTO WA KIKE

Mtendaji wa Kata ya Masengwa wilayani Shinyanga Hussen Majaliwa (kushoto) akiongoza wananchi kupanda miti kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

WANANCHI wa Masengwa wilayani Shinyanga, wameadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa kupanda miti 65 katika Ofisi ya Kata ili kufikisha ujumbe wa kumlinda mtoto wa kike.

Maadhimisho hayo yameongozwa na Mtendaji wa Kata ya Masengwa wilayani Shinyanga Hussen Majaliwa.

Majaliwa akizungumza kwenye maadhimisho hayo, amesema wameamua kuadhimisha siku hizo 16 za kupinga ukatili wa kijinsia kwa kupanda miti, huku wakimfananisha mtoto wa kike anapaswa kutunzwa kama mti na kufikia hatua ya kutoa matunda yani kutimiza ndoto zake.

“Mtoto wa kike anapaswa kutunzwa kama mti, ukiumwagilia ni sawa na kumpatia haki yake ya kielemu, ukiulinda usishambuliwe na mifugo, ni sawa na kumlinda asitongozwe na wanaume na kuambulia ujauzito, ili atimize ndoto zake sawa na mti kutoa matunda,”amesema Majaliwa.

“Wito wangu kwa jamii tumlinde mtoto wa kike kama mti hadi afikie hatua ya kutoa matunda, tuwalinde dhidi ya watu wabaya wala tusiwaozeshe ndoa ya utotoni, ili wafike ndoto zao na kuja kuwa tegemeo katika familia na taifa kwa ujumla,” ameongeza.

Aidha, amesema hali ya mimba za wanafunzi kwenye Kata hiyo kuwa zimekwisha, sababu mwaka huu hakuna hata mimba moja ya mwanafunzi ambayo imeripotiwa.

Nao baadhi ya wananchi akiwamo Hollo Machiya wamesema tatizo ambalo limekuwa likisababisha ukatili dhidi ya watoto wa kike kuendelea katika jamii, linasababishwa na mfumo dume kwa wanaume kutopenda kuwasomesha na kuwageuza vitega uchumi kuwaozesha na kupata utajiri wa mifugo.

Mtendaji wa Kata ya Masengwa wilayani Shinyanga Hussen Majaliwa (kushoto) akiongoza wananchi kupanda miti kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.

Mtendaji wa Kata ya Masengwa wilayani Shinyanga Hussen Majaliwa (kushoto) akiongoza wananchi kupanda miti kuadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.

Zoezi la upandaji miti likiendelea.

Zoezi la upandaji miti likiendelea.

Zoezi la upandaji miti likiendelea.

Zoezi la upandaji miti likiendelea.

Post a Comment

0 Comments