Header Ads Widget

TRA MKOA WA KIKODI KAHAMA WAGUSWA NA WATOTO YATIMA WATOA MSAADAMwakilishi wa kamishna  mkuu kutoka makao makuu TRA Ndositwe  Haonga        akiwa na watoto wanaolelewa  kituo cha watoto yatima wilayani Kahama .    

 Na  Kareny Masasy,Kahama

MAMLAKA ya mapato  Tanzania (TRA ) mkoa wa kodi Kahama   umetoa msaada  vitu mbalimbali  kwa watoto yatima  49 wanao lelewa kwenye kituo cha  KAHAMA  PEACE ORPHAN  CENTER.

Watoto  yatima wanaolelewa hapo  ni kuanzia  umri wa mwaka 0 hadi  miaka 18  kwa kuwapatia malezi ambayo wamekuwa wakiyakosa kama watoto wengine waliopo majumbani.

Mkurugenzi wa kituo hicho  Halima Hamza amepokea msaada   huo leo tarehe 27/Novemba/2022 katika maadhimisho  ya siku ya shukrani kwa mlipa kodi kutoka TRA  huku  akielezea changamoto ya kukosa mfadhili wa kudumu.

Hamza ameeleza  idadi ya watoto alionao kuanzia umri wa mwaka 0 hadi  miwili idadi yao ni saba, na wenye umri kuanzia miaka mitatu hadi  minane idadi yao ni 12 walio baki  idadi yao ni zaidi ya miaka 10.

Hamza amesema changamoto kubwa waliyonayo kituoni hapo ni kukosekana mfadhili wa kudumu nakukosa mahitaji ya muhimu kama chakula ikiwa watoto  28 wanashinda kituoni hapo mchana nakurudi majaumbani mwao  na  watoto 21 wanalala kituoni hapo.

Hamza amesema katika suala la matibabu  baadhi watoto wana bima za afya wengine hawana  wanatumia vibali maalumu vilivyotolewa na ustawi wa jamii kupitia dawati la jinsia.

Msaada ameupokea kutoka TRA  ni mchele kilo 150,  Maharage kilo 30, sukari kilo 40 , mafuta ya kupikia ndoo mbili kubwa,maji katoni 10 ,sabuni katoni moja,mafuta ya kupaka  katoni  tano, madaftri dazani mbili, kalamu za wino  boksi tano, Biskuti kopo kumi na  juisi katoni 10.

Katibu wa kituo hicho  Shabani Mbwana amesema  msaada huo wanashukuru una maana sana kwani watoto wamepata faraja kwani wamekosa malezi na upendo wa karibu kama wanavyopata watoto wengine majumbani.

Mwakilishi wa kamishna  mkuu kutoka makao makuu TRA Ndositwe  Haonga amekabidhi  msaada huo  kwa kutoa shukrani kwa njia hiyo kuwakumbuka makundi maalumu yenye uhitaji ikiwemo kituo cha kulelea watoto yatima.

“Wananchi wanalipa kodi na shukrani yetu  kwao tunaitoa tunairudisha kwa jamii wenye uhitaji  ili watoto nao wajifunze namna ya kulipa kodi pindi wakiwa wakubwa” amesema  Haonga.

Meneja wa TRA mkoa wa kikodi Kahama  Warioba Kanile amesema  leo wameamua kutoa msaada wa vitu katika makundi maalum  kwa kile wanachokipata kwa kuwashukuru walipa kodi na ujumbe wetu ni wananchi walipe kodi kwa  hiari na wajibu wetu kuisaidia jamii hasa makundi maalum.

Tafiti ya TDHMIS 2015/16  inaripoti kuwa  asilimia nane ya watoto  chini ya miaka 18 ni yatima ambayo imeshuka  kutoka asilimia 10 iliyoripotiwa  mwaka 2010  ikiwa wenye umri wa miaka miwili ni asilimia  moja ambapo wamekuwa wakilelewa kwa taratibu mbalimbali.                                                                                     
Watumishi wa mamlaka ya mapato Tanzania TRA mkoa wa kodi Kahama wakishusha bidhaa mbalimbali ambazo wameziandaa kutoa msaada kwenye kituo cha watoto yatima.
Mwakilishi wa kamishna  mkuu kutoka makao makuu TRA Ndositwe  Haonga  akiwa amembeba mmoja wa watoto anayelelewa katika kituo cha watoto yatima.

Maafisa wa TRA mkoa wa kikodi Kahama wakiwa wamebeba watoto wanaolelewa katika kituo cha watoto yatima.
Mwakilishi wa kamishna  mkuu kutoka makao makuu TRA Ndositwe  Haonga  akikabidhi msaada wa vitu mbalimbali  kwa watoto yatima 


 Mmoja wa maafisa kutoka TRA mkoa wa kikodi Kahama akiwa amebeba mtoto  anayelelewa katika kituo cha watoto yatima 

Post a Comment

0 Comments