Header Ads Widget

TRA KAHAMA YAWAPATIA MSAADA WAFUNGWA VIFAA MBALIMBALI

Watumishi wa mamlaka ya mapato Tanzania mkoa wa kikodi Kahama wakiwa ofisini kwao wakijiandaa kwa kutoa msaada,

Na   Neema Sawaka, Kahama

Mwakilishi wa kamishna  mkuu  wa mamlaka ya Mapato Tanzania TRA kutoka makao makuu  Ndositwe  Haonga  amewaongoza  watumishi wa mamlaka  hiyo  wa mkoa wakodi Kahma  kutoa msaada kwa wafungwa.

Msaada huo ni Kandambili,,Sabuni,taulo za kike, dawa za  meno na Miswaki.

Akitoa msaada huo kwa mkaguzi msaidizi  wa gereza  wilayani Kahama Anastazia  Mwamlima  leo  tarehe 27/Novemba/2022 katika maadhimisho ya shukrani kwa mlipa kodi.

Haonga amesema upo utaratibu wa kurudisha shukrani kwa walipa kodi  hivyo watatembelea kwenye makundi maalumu kama vile Magereza na watoto yatima kutoa msaada.

“Pia siku ya kesho tunatarajia kutoa tuzo kwa wafanyabiashara ambao wamekuwa walipa kodi wazuri hilo ni jukumu letu….”amesema  Haonga.

Meneja mkoa wa kodi Kahama Warioba Kanile amesema  wameamua kutoa shukrani kwa njia hiyo  hivyo makundi maalumu yatapokea msaada huo  lengo kudumisha mahusiano na jamii nakuwataka walipe kodi kwa mujibu wa sheria.

Akipokea msaada huo Mwamlima kwa niaba ya mkuu wa gereza  la wilaya hiyo  Hamza Abdala ameshukuru kwa msaada huo kwani wafungwa wengine hawana ndugu wa kuwapatia na huo ndio utakuwa msaada kwao.

“Hapa tunawahifadhia wafungwa pindi wakiwa na shida wamekuwa wakitufuata  nakuwaeleza shida waliyonayo hivyo watasaidiwa kupitia vifaa hivi”amesema  Mwamlima

Watumishi wa mamlaka ya Mapato Tanzania mkoa wa kikodi Kahama  wakionyesha bango lenye ujumbe 


Mwakilishi wa kamishna  mkuu  wa mamlaka ya Mapato Tanzania TRA kutoka makao makuu  Ndositwe  Haonga   wa pili kutoka kushoto akiwa na meneja wa mkoa wa kikodi Kahama  Warioba Kanile aliyevaa kofia,

Baadhi y watumishi wa mamlaka ya mapato Tanzania mkoa wa kodi Kahama wakiwa eneo la gereza wilayani Kahama

Mwakilishi wa kamishna  mkuu  wa mamlaka ya Mapato Tanzania TRA kutoka makao makuu  Ndositwe  Haonga   akizungumza walivyoguswa kutoa msaada kwa wafungwa katika gereza la wilaya ya Kahama

Mkaguzi msaidizi wa maregeza ya wilaya Kahama Anastazia  Mwamlima akisalimiana na maafisa wa TRA.
 Meneja wa mamlaka ya Mapato TRA mkoa wa kikodi Kahama   pamoja na Mwakilishi wa kamishna  mkuu  wa mamlaka ya Mapato Tanzania TRA kutoka makao makuu  Ndositwe  Haonga   wakisalimiana na mkuu wa gereza wilaya ya Kahama Hamza Abdallah.

Mwakilishi wa kamishna  mkuu  wa mamlaka ya Mapato Tanzania TRA kutoka makao makuu  Ndositwe  Haonga  akisalimiana na mkaguzi wa gereza  Anastazia Mwamlima.

Watimishi wa mamlaka ya mapato Tanzania TRA mkoa wa kodi Kahama wakiwa eneo la ofisini 


Watumishi wa mamlaka ya mapato TRA mkoa wa kikodi Kahama wakijiandaa na utoaji wa msaada.

Picha zote na Kareny  Masasy

Post a Comment

0 Comments