` MONGELLA: MKOA WA SHINYANGA NI NGUZO KUU YA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM

WANDAMAN HOTEL

MONGELLA: MKOA WA SHINYANGA NI NGUZO KUU YA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM

 

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara John Mongella, amesema Mkoa wa Shinyanga ni kati ya mikoa mikubwa ambayo chama hicho kinautegemea kama nguzo, huku akisisitiza kasi ya maendeleo iendane na idadi ya wabunge 11 waliopo mkoani humo.

TAZAMA VIDEO👇👇


Mongella, ambaye pia ni mlezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Shinyanga, amebainisha hayo leo Julai 17, 2026, kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM mkoani humo.

Amesema, kutokana na mkoa huo kuwa ni miongoni mwa mikoa ambayo ni nguzo ya chama hicho, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan na Mwenyekiti wa CCM Taifa, amekuwa akiweka nguvu kubwa ya kuleta kasi ya maendeleo kwa wananchi.
“Mkoa wa Shinyanga una takribani Wabunge 11 na ni mkoa ambao una uwakilishi mkubwa bungeni, hivyo lazima kasi ya maendeleo katika mkoa huo ionyeshe wingi huo,” amesema Mongella.

Amewataka pia wana-CCM na viongozi wa mkoa huo kuendelea kushikamana, kuwa na umoja, kudumisha amani, pamoja na kukiimarisha chama ili kiendelee kuwa na nguvu zaidi.
Naye Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa, amesema kuwa wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM ya mkoa huo, wana uwezo mkubwa katika kukijenga chama.

Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga na Naibu Waziri wa Nishati Salome Makamba, akizungumza kwa niaba ya wabunge wote, amesema wataendelea kuchapa kazi kwa kumsaidia Rais Samia, pamoja na kupeperusha bendera ya mkoa wa Shinyanga, na watakuwa wawakilishi wazuri bungeni.
Amesema ni fahari kubwa kwao kuwa na uwakilishi mkubwa bungeni, na kwamba watamweka vizuri mlezi wao John Mongella katika medali nzuri, kuwa analea viongozi makini, wenye heshima, adabu, na walio waaminifu kwa Chama cha Mapinduzi.

Ameongeza kuwa watafanya kazi ya kukijenga chama, kufanya kazi za Serikali, na kuweka umoja wa watanzania wote, kwa maslahi mapana ya chama na watanzania kwa ujumla.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita, amesema mkoa huo ni shwari kiusalama, pamoja na usalama wa chakula, na wamekuwa wakifanya kazi kwa kushirikiana na Chama, katika kuhakikisha wanawaletea maendeleo wananchi kwa kuzingatia ilani ya CCM.

TAZAMA PICHA👇👇
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara John Mongella akizungumza.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara John Mongella akizungumza.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara John Mongella akizungumza.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akizungumza.
Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Odilia Batimayo akizungumza.
Mbunge wa Vitimaalumu Mkoa wa Shinyanga na Naibu Waziri wa Nishati Salome Makamba akizungumza.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita akizungumza.

Kama una Taarifa, Habari, Tangazo n.k Wasiliana nasi kupitia shinyapress@gmail.com au +255 788 469 464