Header Ads Widget

UTPC YAWAJENGEA UWEZO VIONGOZI WA KLABU ZA WAANDISHI WA HABARI MATUMIZI SAHIHI YA FEDHA NA UTAWALA BORA


Paulo Malimbo, Mwezeshaji mambo ya uongozi na utawala bora.

Rais wa UTPC Deogratius Nsokolo akizungumza kwenye mafunzo hayo.

Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.

Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.

Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.

Washiriki wakiwa kwenye mafunzo.

Na Frank Mshana, DODOMA

Umoja wa Klabu za waandishi wa habari Tanzania (UTPC) umeendesha semina ya siku tatu ya kuwajengea uwezo viongozi wa klabu, yenye lengo la kuwajengea uwezo wa kusimamia matumizi ya fedha na vifaa wezeshi vya klabu zao.

Akizungumza wakati wa uzindunzi wa semina Mwenyekiti wa maadili na mafunzo kutoka UTPC Frank Leonard, amesema Press Club nyingi nchini zimekuwa na changamoto kubwa kwenye usimamizi wa matumizi ya fedha ikiwa ni pamoja na matumizi mabaya na raslimali zingine hali ambayo imekuwa kikwazo kwa wanachama kutekekeza majukumu yao.

Aidha ameongeza kuwa changamoto hizo ambazo zimekuwa zikisababisha migogoro, kushindwa kuendesha ofisi na udanganyifu wa baadhi ya viongozi kwenye upande wa matumizi ya fedha na matumizi ya raslimali imekuwa ikiwakatisha tamaa wafadhili ambao wanaiwezesha UTPC.

Akitoa mada ya matumizi sahihi ya fedha, Paulo Malimbo mwezeshaji wa mambo ya uongozi na utawala bora kutoka Baraza la Habari Tanzania amesema ili kuoata mafanikio na kusonga mbely ni lazima matumizi ya fedha yasimamiwe kulingana na mahitaji sahihi na kuweka taarifa sahihi ya matumizi kama kumbukumbu ili kuepuka matumizi mabaya ya fedha.

Aidha, wawa Saidi ni mwezeshaji katika upande wa usimamizi wa fedha amezitaka Press club kuanzisha miradi inayoendana na taaluma ya uandishi wa habari kama Online Tv na Bolgs na.kuziendeleza kama vyanzo vya mapato hali itakayokuwa ni alama ya Press Club kwa wadau.

Rais wa Umoja wa Klab za waandishi wa habari (UTPC) Bwana Deogratias Nsokolo amesema ni lazima Viongozi na wanachama wa Press Clubs kukubaliana na mabadikiko ya Katiba na miongozo ya UTPC huku akisisitiza waratibu na makatibu kuwa makini sana katika maeneo ya utunzaji wa kumbukumbu na matumizi ya fedha huku akiwaomba wenyeviti kuzingatia swala la utawala bora.

Post a Comment

0 Comments