Header Ads Widget

DC MBONEKO AKAGUA UJENZI VYUMBA MADARASA, RAIS SAMIA APONGEZWA

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akishiriki kujenga vyumba vya madarasa katika Shule mpya ya Sekondari Salawe wilayani Shinyanga.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MKUU wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, amekagua ujenzi wa vyumba vya madarasa, ambavyo vilitolewa fedha na Rais Samia Suluhu Hassan, kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha kwanza mwakani.

Mboneko amefanya ziara hiyo leo Novemba 9, 2022 kukagua ujenzi wa vyumba hivyo vya madarasa, katika halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga na wilaya ya Shinyanga, ili kuona utekelezaji wa miradi hiyo.

Amesema amefanya ziara hiyo kuona hatua ya ujenzi wa vyumba hivyo vya madarasa, ili vikamilike kwa wakati na ubora unaotakiwa kwa kuendana na thamani halisi ya fedha (value for money), na mwakani vianze kutumika kufundishia wanafunzi.

"Rais Samia katika halmashauri zetu hizi mbili ametoa kiasi cha fedha Sh. bilioni 2.2 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 109, Manispaa ya Shinyanga vyumba 61wilaya ya Shinyanga vyumba 45, na kasi yake ya ujenzi ni nzuri na wanafunzi watayatumia mwakani," amesema Mboneko.

Aidha, amesema wanafunzi wote ambao watachaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwakani wote wahudhulia shule na hakuna hata mmoja kukosa, ikiwa elimu ni bure na wasome kwa bidii na kutimiza ndoto zao.

Nao baadhi ya madiwani akiwamo Mussa Andrew wa Kolandoto na Awadhi Mbaraka wa Solwa, wamemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha na kufanikisha ujenzi huo wa vyumba vya madarasa ambavyo vitatumiwa na wanafunzi wa kidato cha kwanza mwakani ili wasome katika mazingira Rafiki.

Naye Mkuu wa shule ya Sekondari Kolandoto Manispaa ya Shinyanga Deus Maganga, amesema madarasa Saba ambayo wamepewa na Rais Samia Shuleni hapo yamemaliza kabisa upungufu uliopo na wanafunzi watasoma bila ya kubanana.

Nao wanafunzi akiwamo Josephine Juma kutoka Kolandoto Sekondari, wamesema wanaposoma kwa kujinafasi hata masomo wanaelewa vizuri, kuliko kusoma kwa kubanana ambapo inakuwa vigumu kuelewa masomo na hatimaye kufanya vibaya kutaaluma.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumzia ziara yake ya kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa, kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha kwanza mwakani.

Diwani wa Solwa Awadhi Mbaraka akitoa pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan kutoa fedha za ujenzi wa vyumba vya madarasa, pamoja na usimamizi mzuri wa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko kuhakikisha madarasa hayo yana kamilika kwa wakati.

Mkuu wa shule ya Sekondari Kolandoto Deus Maganga akielezea namna vyumba 7 vya madarasa shuleni hapo vitakavyo maliza upungufu na wanafunzi kusoma kwa nafasi.

Mwanafunzi Patric Shija wa shule ya Sekondari Kolandoto akielezea umuhimu wa vyumba vipya vya madarasa shuleni hapo.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akishiriki kwenye ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule mpya ya Sekondari Solwa wilayani Shinyanga kwa kufyatua matofali.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akiendelea kufyatua matofali katika shule mpya ya Sekondari Solwa wilayani Shinyanga.

Diwani wa Solwa Awadhi Mbaraka akishiriki na yeye kufyatua matofali katika shule mpya ya Sekondari Solwa.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akishiriki ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule mpya ya Sekondari Salawe.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akikagua ubora wa matofari.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akikagua ubora wa matofari.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akikagua ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya Sekondari Kolandoto Manispaa ya Shinyanga.

Ujenzi wa vyumba vya madarasa shule ya Sekondari Kolandoto ukiendelea.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akikagua ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule mpya ya Sekondari Solwa wilayani Shinyanga.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akikagua ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule mpya ya Sekondari Solwa wilayani Shinyanga.

Muonekano wa ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule mpya ya Sekondari Solwa wilayani Shinyanga.

Ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule mpya ya Sekondari Solwa ukiendelea.

ujenzi wa darasa katika shule ya Sekondari Ghembe wilayani Shinyanga ukiendelea.

Ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya Sekondari Iselamagazi wilayani Shinyanga ukiendelea.

Post a Comment

0 Comments