Header Ads Widget

MISA-TAN YAENDESHA MAFUNZO UHURU WA KUJIELEZA KWA WANAHABARI

Marko Gideon akitoa mafunzo ya uhuru wa kujieleza kwa Wanahabari yaliyoratibiwa na Misa-Tan.

Na Marco Maduhu, SINGIDA

WANAHABARI wapatao 40 kutoka Mikoa ya Tabora, Dodoma, Shinyanga, Simiyu na Singida, wamepewa mafunzo ya kuandika habari za kukuza uhuru wa kujieleza.

Mafunzo hayo yameanza kutolewa leo Novemba 3, 2022 mkoani Singida ambayo yatachukua muda wa siku tatu, yakiratibiwa na Taasisi ya vyombo vya habari kusini mwa Afrika Tawi la Tanzania( Misa-Tan), kwa ufadhili wa ubalozi wa Kanada nchini Tanzania.

Mwezeshaji wa mafunzo hayo Marko Gideon, amesema mafunzo hayo yametolewa mara baada ya kufanyika utafiti na kubainika kuwa habari za uhuru wa kujieleza hapa nchini zimekosekana.

"Unapokosekana uhuru wa kujieleza, utawala wa Sheria hautakuwepo, uwajibikaji wa viongozi, hakutakuwa na usawa wa kisheria, hakuna uwazi, uchaguzi hauwezi kuwa huru na haki, wala kudhibiti matumizi mabaya ya viongozi," amesema Gideon.

Naye Andrew Marawiti kutoka Misa-Tan, amesema baada ya mafunzo hayo wanatarajia kuona Wanahabari wakiandika habari nyingi zinazohusu uhuru wa kujieleza.

Nao baadhi ya Wanahabari walioshiriki mafunzo hayo, wamesema wanatarajia kuwaongezea maarifa zaidi wakati wa utekelezaji wa majukumu yao ya uandishi wa habari.

Marko Gideon akitoa mafunzo ya uhuru wa kujieleza kwa Wanahabari yaliyo ratibiwa na Misa-Tan.

Andrew Marawiti kutoka Misa-Tan akizungumza kwenye mafunzo hayo.

Waandishi wa habari wakiwa kwenye mafunzo.

Post a Comment

0 Comments