Header Ads Widget

WAZAZI WATAKIWA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUONDOA CHANGAMOTO SHULENI





Wahitimu wa  kidato cha nne shule ya sekondari Nyandekwa manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga.

Na  mwandishi wetu

Wazazi  kata ya Nyandekwa manispaa ya Kahama  wametakiwa kushirikiana na serikali  ili kuondoa changmoto zinazowakabili wanafunzi  na walimu shuleni ikiwemo ujenzi wa matundu ya vyoo na nyumba za walimu.

Mgeni rasmi  Emanuel Ntonge  ambaye ni mstaafu wa chuo  cha uhasibu Tabora ameyasema hayo  jana kwenye mahafali ya  13 ya kidato cha nne  katika shule ya sekondari Nyandekwa.

Ntonge  amewataka wahitimu  wanapo kuwa nyumbani wawe na maadili  mema na kutojiingiza kwenye makundi maovu.

Ntonge amewataka  wanafunzi  wanaobaki kuachana na tabia za utoro  nakuwasihi  wasome kwa bidii  ili kuweza kufikia  malengo yao kwani ada na michango mingine imeondolewa na serikali.

Mkuu wa shule hiyo  Kiseka kallam amesema  kuna  wahitimu 90  kwa mwaka huu na wamejipanga  vyema kufanya mtihani mwezi ujao.

Aidha risala ya wanafunzi  iliyosomwa na Magreth Elias wameomba serikali  masomo yafundishwe kwa lugha ya Kiswahili ili waweze kuelewa.








Mgeni rasmi akiingia  nakuwasalimia  waalikwa

Wahitimu wakisikiliza wosia kutoka kwa mgeni rasmi





Mhitimu  akisoma risala

Mgeni rasmi Emanuel Ntonge akipokea risala kutoka kwa wahitimu 

Wahitimu wa kidato cha nne wakiingia ukumbuni


Post a Comment

0 Comments