Header Ads Widget

MTAALAMU AELEZA KANISANI UMUHIMU WA LISHE KWA SIKU 1000 ZA MTOTO.


 

Kaimu ofisa lishe halmashauri ya Msalala  wilayani Kahama mkoani Shinyanga akieleza kanisani maana ya siku 1000  za mtoto   kuanza kupata lishe bora.

Na Kareny  Masasy, Kahama

WAUMINI wa kanisa la kisabato SDA  Igomela wilayani Kahama wamepewa somo la lishe katika maandalizi ya ujauzito  huaza kabla ya miezi sita  na kumtengeneza mtoto aliye bora.

Kaimu ofisa lishe wa halmashauri ya Msalala  wilayani Kahama Peter Shimba amesema hayo jana kwenye  kongamano la mafundisho  ya afya  kwa waumini wa kanisa la  Kisabato katika kanisa la Igomelo SDA .

Shimba amesema wajawazito wengi wanapopata ujauzito huanza kusema wanajisikia vibaya hali hiyo inatokana na mama huyo kukosa maandalizi ya lishe tangu awali kabla ya kubeba ujauzito huo.

Shimba amesema baadhi ya  mama wengi wanabeba mimba wanasema ni bahati mbaya  dhana hiyo waondoe wafanye maandalizi  ya lishe kwanza  ili kuweza kuwa na mtoto aliyebora…..

“Kila mzazi anapenda kuwa na mtoto bora na mtoto bora huanza kutengenezwa  kwa kupata lishe bora kabla ya kuzaliwa na baada ya kuzaliwa  ndipo inafikisha  siku 1000”amesema Shimba.

Shimba akifafanua  faida  za rangi  tano  za mboga ya majani  na matunda   katika  mwili ili kuepukana na magonjwa na kuongeza kinga mwilini.

“Mkoa wa Shinyanga  kwa tafiti zilizotolewa na Tanzanaia  Demographic  Health Suvey  (TDHS) mwaka 2018  zinaeleza  udumavu  kwa watoto ni  asilimia 32”.

 Mzee wa kanisa  hilo Bazwanje  Wilbert amesema  kanisani hapo huwa   wanasomo la afya ambapo leo  wamempata ofisa lishe na kutoa elimu ya lishe  wameelewa   umuhimi wa afya  kwa kipengele cha lishe  kwa watoto na wajawazito.

 “Ili kuifanya Tanzania kuwa na watoto  bora lazima tuwapatie watoto wetu lishe bora na kuhimiza wazazi kunyonyesha  muda wa miaka miwili”amesema  Wilbert.

Muumini Dinna Mnyoro  ameelewa siku 1000 tangu mama anapobeba ujauzito na  mtaalamu huyo kufafanua  mboga za majani  na matunda ni kitu muhimu kwa  wazazi  nafikiri wamemuelewa vizuri kuwa rangi tano zote kwenye mboga za majani ni muhimu mwilini.

 

kaimu ofisa lishe halmashauri ya Msalala   wilayani Kahama Peter Shimba akiwa kwenye kongamano la mafunzo juu ya afya akitoa elimu ya lishe kwa waumini 
Vijana wakisikiliza somo la lishe kanisani.


Waumini wa kanisa la  wasabato  Igomela  SDA  wilayani Kahama. mkoani Shinyanga.

Mhudumu wa  kanisa la SDA kanisa la Igomelo  Yona  Machibya akielezea umuhimu wa kongamono  kwa kupata elimu za afya mbalimbali.


viongozi wakiwa meza kuu wakijiandaa na kongamano

Post a Comment

0 Comments