Header Ads Widget

DC KAHAMA AZIONYA HALMASHAURI KUCHELEWESHA FEDHA ZA LISHE ZILIZOTENGWA KWA AJILI YA WATOTO


Mkuu wa wilaya ya Kahama  mkoani Shinyanga Festo Kiswaga  akifanya  makabidhiano ya pikipiki na kaimu afisa lishe wa halmashauri ya Msalala Peter Shimba .

Na Kareny  Masasy, Msalala

MKUU  wa wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga Festo Kiswaga amezitaka halmashauri kuhakikisha zinatoa   sh 1,000  zilizotengwa kwa ajili ya watoto kwenye masuala ya  lishe  na kutoona alama nyekundu ikimaanisha kufanya vibaya kwenye kadi..

 

Kiswaga amesema hayo leo tarehe 17/010/2022   alipokuwa akikabidhi pikipiki  kwa afisa lishe, afisa afya na mratibu  wa huduma ngazi ya jamii  katika halmashauri ya Msalala zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu  alipokuwa akisaini mkataba wa lishe.

Kiswaga amesema   pikipiki hizo wazitumie kufanya kazi kwa bidii kama ilivyoagizwa na Rais  Samia Suluhu  ambapo mkataba huo naye alisainishwa kutoka kwa mkuu wa mkoa Sophia Mjema  nakuzitaka halmashauri  za Ushetu na Msalala zisiwe nyuma katika masuala ya lishe na fedha walizozitenga zitolewe kwa wakati .

“Tumeweka mikataba hivyo  wakurugezi  washuke kwa watendaji wa kata  pikipiki hizi  wamepewa waweze kufuatilia ziwanufaishe wananchi na  sh 1000 zinazokatwa kwaajili ya watoto kuhusu lishe zifike kwa wakati kulikuwepo na ucheleweshwaji”amesema Kiswaga.

Kiswaga amesema hataki  kupata alama nyekundu kwenye kadi  katika wilaya yake kwenye halmashauri  zote akikuta hivyo muhusika ajiandae kuacha kazi  huo utakuwa ni uzembe maana kitendea kazi unacho mafuta na  ukarabati vyote vinawezeshwa na serikali.

Kaimu ofisa Lishe halmashauri ya Msalala  Peter Shimba amesema   wametenga  zaidi ya  sh Millioni 61.5 mapato ya ndani kwaajili ya lishe kwa watoto katika bajeti ya mwaka 2022/2023.

 Shimba  amesema   viashiria  vya ukosefu wa lishe huvitazama  kwa mjamzito sababu ndiye amebeba mtoto nakumtegemea katika ukuaji wake.

Shimba  amesema   miezi ya kuzingati  ulaji mzuri kwa mtoto ni kuanzia umri wa miezi 0 hadi 23 akikosa  hapo  mtoto akipata udumavu ni  vigumu kumrekebisha na kurudi kwenye hali nzuri.

Shimba amesema  watoto kwa mwaka jana waliozaliwa na uzito wa chini ya kg 2.5 ni 57 sawa na asilimia 0.1.

“Halmashauri ya Msalala ina Upungufu wa damu kwa wajawazito asilimia 4.2,  ambapo kiwango cha udumavu kwa mkoa ni asilimia 32 ukondefu asilimia  4  na uzito pungufu ni asilimia  15"amesema Shimba.

Shimba amesema kazi ya afisa lishe  ni kushughulikia  mjamzito anapata  lishe bora  wakati wote katika  siku  1000  tangu anapopata ujauzito  na mtoto kunyonyeshwa maziwa ya mama  hadi miaka miwili mfululizo.

Ofisa afya halmashauri ya Msalala  Marthad Khojama  amesema  kupata usafiri atahakikisha wajawazito na watoto wanatembelewa kwenye maeneo yao  kwa  urahisi  kwaajili ya kuhamasisha ulaji wa lishe bora  katika hali ya usafi ,uwepo wa madini joto na utumiaji wa vyoo bora.

Pikipiki zikikabidhiwa kwa afisa lishe, afisa afya na mratibu mhudumu ngazi ya jamii   halmashauri ya Msalala.
kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya Msalala Solomon  Zedekia   akishuhudia makabidhano kati ya afisa lishe,afisa afya na mratibu mhudumu ngazi ya hamii  na mkuu wa wilaya Festo Kiswaga.
Mkuu wa wilaya ya Kahama akizikagua pikipiki nakutoa maelezo.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga akitoa maelekezo 
Zoezi la ukaguzi pikipiki likiendelea kabla ya kukabidhi mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga.
Makabidhiano yakifanyika.

Post a Comment

0 Comments