Header Ads Widget

RAIS SAMIA ATANGAZA MATOKEO YA SENSA WATANZANIA TUPO MILIONI 61, 741,120 WANAWAKE WANAONGOZA KWA IDADI KUBWA

Idadi ya Watanzania ni 61,741,120

Idadi ya Watanzania ni 61,741,120


Hayo yamebainishwa na Rais Samia Suluhu Hassan, muda mfupi uliopita wakati akitangaza matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022 iliyofanyika kuanzia Agosti 23 mwaka huu.

Amesema watu 59,851,357 wapo Tanzanzia Bara na watu 1,889,773 wapo Tanzania Zanzibar.

Kuhusu idadi hiyo wanawake wapo 31,687,990 sawa na asilimia 51 ya watu wote na wanaume ni 30,530,130 sawa na asilimia 49 ya watu.

Sensa ya watu na makazi ni utaratibu wa kukusanya, kuchambua, kutathimini, kuchapisha na kusambaza takwimu za kidemographia, kiuchumi na kijamii kuhusiana na watu wote na makazi yao katika nchi kwa kipindi maalumu.

Sensa hufanyika kila baada ya miaka 10, ambapo sensa ya mwaka 2022 ni ya sita kufanyika nchini baada ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964. Sensa nyingine zilifanyika mwaka 1967, 1978, 1988, 2002 na 2012. Matokeo ya sensa ya mwaka 2012 yalionesha kuwa Tanzania ilikuwa na watu 44,929,002 wakiwamo 43,625,434 Tanzania Bara na 1,303,568 Zanzibari.
 
Chanzo habari leo
 

Post a Comment

0 Comments