Header Ads Widget

AOMBA MSAADA WA MATIBABU

MZEE SHIJA KAHEZA SENGEREMA MZALIWA WA KIJIJI CHA KASAMWA MKOANI GEITA AMBAYE KWA SASA ANAISHI MTAA WA MSHIKAMANO MANISPAA YA SHINYANGA.

ANAOMBA MSAADA WA MATIBABU YA MGUU NA KIBOFU CHA MKOJO BAADA YA KUUGUA KWA ZAIDI YA MIAKA 15 NA KUTIBIWA KATIKA HOSPITALI MBALIMBALI BILA MAFANIKIO IKIWEMO HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA SHINYANGA NA HOSPITALI YA RUFAA KANDA BUGANDO.

HALI AMBAYO IMESABABISHA AANDIKIWE KUKATWA MGUU BAADA YA KUPATA MADHARA MAKUBWA YA KUVIMBA NA MAUMIVU MAKALI SEHEMU ZA KIUNO NA MIGUU.

AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI WALIOMTEMBELEA NYUMBANI KWA DADA YAKE AMBAPO ANAPATIWA MSAADA KWA MUDA MZEE SHIJA AMEELEZA KUWA MWAKA 2009 MGUU WA KE ULIOTA KIPELE SEHEMU YA CHINI YA KISIGINO NA KUANZA KMUWASHA NA ALIPOKIKWANGUA KIPELE HICHO NDIO UKAWA MWANZO WA MGUU KUPATA KIDONDA KILICHOENDELEA KUCHIMBIKA SIKU BAADA YA SIKU HADI KUFIKIA MFUPA HUKU AKIPATA MAUMIVU MAKALI.

AMEENDELEA KUELEZA KUWA AMETIBIWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA SENGEREMA NA BAADAE HOSPITALI YA MKOA WA GEITA LAKINI HALI ILISHINDI NA NDUGU ZAKE KUMCHUKUA NA KUMFIKISHA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA SHINYANGA KWA AJILI YA MATIBABU ZAIDI.

AMESEMA AMETIBIWA KWA ZAIDI YA MIEZI MITATU KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA SHINYANGA NA BAADAE KUPEWA RUFAA YA KWENDA KWENYE HOSPITALI YA KANDA YA BUGANDO JIJINI MWANZA AMBAPO ALITIBIWA KWA MUDA BILA MAFANIKIO AMBAPO ALIANDIKIWA KUKATWA MGUU NA KUTAKIWA KULIPA ZAIDI YA SHILINGI 1,500,000 KAMA GHARAMA ZA KUKATA MGUU TOFAUT NA GHARAMA ZA HUDUMA ZINGINE ZA KITANDA,DAWA NA CHAKULA AMBAZO JUMLA YAKE ZIKIWA TAKRIBAN SHILINGI MILIONI 3.

KUTOKANA NA HALI HIYO MZEE SHIJA MAHEZA SENGEREMA AMBAYE HANA MTOTO NA KWA SASA AMEKIMBIWA NA MKE HUKU AKITEGEMEA MSAADA KUTOKA KWA MAJIRANI ANAOMBA MSAADA WA HALI NA MALI ILI AKAPATE MATIBABU IKIWA NI PAMOJA NA KUKATWA MGUU KABLA HAUJAENDELEA KUFANYA MADHARA MAKUBWA ZAIDI.

KWA YEYOTE ATAKAYEGUSWA NA CHANGAMOTO YA MGONJWA SHIJA KAHEZA SENGEREMA ATOE MSAADA KWA KUTUMIA NAMBA ZA SIMU 0768947948 NA 0699257664 JINA LITAKUJA SHIJA KAHEZA.
AHSANTENI SANA KWA MSAADA WENU

Mzee Shija Kaheza Sengerema

Post a Comment

0 Comments