Header Ads Widget

JESHI LA POLISI LINAWASHIKILIA WATU 13 KWA TUHUMA YA KUHUJUMU MIUNDOMBINU YA UMEME KUTOKA TANESCO


 Kamanda wa  polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi akionesha vifaa vilivyohujumiwa kutoka kwenye miundombinu ya shirika la umeme  Tanzania (Tanesco)

Na  Kareny  Masasy,Kahama

JESHI  la polisi mkoani Shinyanga linawashikilia watu 13 kwa tuhuma ya kuhujumu  miundombinu ya nishati ya umeme yenye thamani ya zaidi ya sh Millioni 10 kutoka shirika la umeme nchini (Tanesco) wilayani Kahama.

Walioshikiliwa  majina yao yamehifadhiwa ni wananchi wa kawaida saba wakiwemo viongozi wa dini,watumishi wa shirila la umeme Tanesco wawili na vishoka wanne .

Kamanda wa  polisi mkoani Shinyanga  Janeth  Magomi ameeleza leo  waandishi wa habari tarehe 30/09/2022  kuwa  mnamo tarehe  25/09/2022 na tarehe 29/09/2022 polisi kwa kushirikiana  na maafisa  kutoka Tanesco  liliendesha oparesheni  maalum iliyolenga kufichua vitendo vya kihalifu vinavyohusisha uhujumu wa miundombinu.

 Kamanda Magomi amesema  kuwa  jumla ya Transfoma  73  za Tanesco wilayani Kahama zimehujumiwa  kwa kukatwa wire wa earth rod na kuibiwa earth rod zenyewe hivyo kuhatarisha  usalama wa miundombinu hiyo.

“Vitendo  hivi ni kinyume cha sheria na vinalikosesha  shirika mapato,watuhumiwa  ambao ni watumishi wa shirika hilo  walikuwa wakishirikiana  na vishoka  kufanya vitendo vya kuhujumu miundombinu ya shirika  kwa kuiba vifaa na kuwaunganishia  wateja  bila kufuata utaratibu”amesema  Kamanda Magomi.

Kamanda Magomi amesema   upelelezi unaendelea na  wakibainika watafikishwa mahakamai  na kutoa  wito kwa wananchi  wote  wa mkoa wa Shinyanga  kuacha tabia  hiyo mara moja  na yeyote atakaye bainika atachukuliwa hatua za kisheria

Kaimu Meneja wa Tanesco  wilaya ya Kahama Mhandisi Tumaini Chonya  amesema  kuwa  watuhumiwa hao wameiba boksi na kuunganishia nyaya  ambapo  wanatumia  bila kulipia umeme lakini pia ni hatari  kwa sababu inakuwa haina earth rod wakati wa masika kipindi cha mvua  radi ikija inaweza kuunguza nyumba na kusababisha hasara kwa mtumiaji huyo na shirika pia.

“Baadhi ya watumishi wetu wenyewe ndiyo wanafanya mchezo huo lengo lao ni kutumia tu bila kulipia muda wote na wewe mwananchi ukiona hivyo   kwanini usishtuke  hujuma hiyo inaongeza gharama kwenye shirika kurudishia  miundombinu hiyo sasa haikubaliki wananchi mshtuke  unatumiaje umeme wa luku bila kuisha muda wote?”amesema   Chonja.

Kaimu meneja kutoka shirika la umeme Tanzania( Tanesco) wilayani Kahama Mhandisi Tumaini Chonya akiangalia vifaa kutoka shirika hilo.

Kamanda wa polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi akiangalia vifaa vya umeme vilivyohujumiwa

Kamanda wa polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi akiangalia nyaya za umeme zilizohujumiwa pamoja na rimoti za luku.

Kamanda wa Polisi Janeth Magomi akitoa taarifa.


Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Janeth Magomi akionesha vifaa.
Vifaa vilivyo hujumiwa vilivyo toka kwenye shirika la umeme Tanesco

Vifaa vilivyodaiwa kuhujumiwa kutoka Tanesco.

Post a Comment

0 Comments