Header Ads Widget

ASKOFU MABUSHI AWATAKA WAZAZI KUACHA TABIA YA KUWAFUGA WATOTO BALI WAWALEEASKOFU   MABUSHI  AWATAKA WAZAZI KUACHA  TABIA YA KUWAFUGA WATOTO   BALI WAWALEE

Na Kareny Masasy

WAZAZI na walezi wa manispaa ya Shinyanga wameaswa kuachana na tabia ya kuwafunga watoto kama wanyama bali wawe  wanawalea kwenye kutazama malezi zaidi  wawapo  majumbani.

Hayo yamesemwa leo tarehe 21/08/2022 na askofu  David Mabushi wa   Kanisa la International Evangelical Assemblies of God Tanzania,lililopo  manispaa ya Shinyanga katika ibada ya jumapili,wakati akitoa mahubiri kwa  maandalizi ya wiki  ya watoto kwa kanisa hilo.

Mabushi  amesema wazazi na walezi wamekuwa na tabia ya kuwafanya watoto kama mifugo na kutowalea kwa msingi bora ya kidini na malezi  yaliyo muhimu ya jamii  matokeo yake wamejikita  kufuatilia chakula na malazi  tu.

Mabushi  amesema  wazazi hawana muda na watoto na badaye kuwalaumu kuwa kizazi cha siku hizi kina shida,jukumu la wazazi ni kufatilia mwenendo wa watoto na kuwapa adhabu zinazostahili ili waondokane na ujinga na matendo maovu yasiyofa kwa Mungu na jamii.

"Tuna mchango gani kwa watoto wetu kama hatuweki muda wa kufatilia tabia na mienendo yao,tuko bize na kuwatafutia chakula na malazi kama mifugo tu,tunawafanya watoto kuwa mifugo na hakuna muda wa majadiliano na kufundishana maadili ya dini na jamii"

Kwa upande wake,Mama mchungaji wa kanisa hilo,Suzani Mabushi  amesema mikoa ya kanda ya ziwa baadhi ya   wazazi na walezi  hawana msukumo wa kupeleka watoto shule na kuwapatia mafunzo ya dini,  ukilinganisha na mikoa ya kasikazini.Pia wazazi na walezi wa kanda ya ziwa wanaona mafunzo ya dini  sio lazima. 

"Watoto tukae nao wenyewe wajue hali ya mzazi ikoje  kwa mazingira yoyote  tusiwapeleke wakakaa hovyo ndugu wengine sio watu wazuri" anasema suzani.

Ngatale Peter muumini wa kanisa hilo  amesema kuwa  changamoto iliyopo kwa sasa  ya kuwalea watoto  hovyo ni jambo  linalosababisha   kuwepo na athari za  vitendo vya ukatili  ni vyema kuwakumbuka watoto katika malezi.

mwisho.
Post a Comment

0 Comments