Header Ads Widget

KAHAMA WAUPIGA MWINGI MIRADI YA MAENDELEO IKIZINDULIWA NA MWENGE WA UHURU KWA KISHINDO NA KUWEKWA JIWE LA MSINGI

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Sahili Nyanzabara Geraruma akizindua mradi wa maji safi na salama kutoka Ziwa Victoria wa Ngogwa- Kitwana katika Manispaa ya Kahama.

Na Marco Maduhu, KAHAMA

KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa (2022) Sahili Nyanzabara Geraruma, amezindua Miradi ya Maendeleo pamoja na kuweka mawe ya Msingi katika Halmashauri ya Manispaa ya Kahama.

Mwenge wa Uhuru leo Julai 30 umekimbizwa katika Manispaa ya Kahama, ukitokea Halmashauri ya Msalala, ambapo umepitia Miradi Mitano ya Maendeleo yenye thamani ya Sh. bilioni 4.9.

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa Miradi hiyo, Sahili amesema Miradi yote ni mizuri na na ndiyo maana ameridhia kuizindua na kuweka mawe ya msingi.

"Nimekagua Miradi yote ni mizuri Kahama mmeupiga Mwingi, endeleeni hivyo hivyo kutekeleza Miradi na kuboresha huduma kwa wananchi," amesema Geraruma.

Aidha, awali akizindua mradi wa Majisafi na salama wa Ngogwa-Kitwana ,ambao umetekelezwa kwa ushirikiano wa Mamlaka mbili za Maji, (SHUWASA), (KUWASA) na Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA), amewataka wananchi kuitunza miundombinu hiyo ya Maji ili nayo iwatunze na kuendelea kupata huduma ya safi.

Pia akiwa katika ujenzi wa Jengo la uchunguzi la Magonjwa katika Hospitali ya Manispaa ya Kahama, amewapongeza wa ujenzi huo ambao utasaidia wananchi wa Kahama kupata huduma ya matibabu karibu na kuacha kusafiri kwenda Bugando Jijini Mwanza au Muhimbili Dar es Salaam.

Katika hatua nyingine amewaasa wananchi wa Kahama, kuwa siku ya kuhesabiwa Sensa ya watu na makazi, siku hiyo wajitokeze kwa wingi kuhesabiwa na kutimizia malengo ya Serikali kupata idadi ya watu wake.

Awali Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama Clement Mkusa, amesema Mwenge huo wa Uhuru katika Manispaa hiyo utakimbizwa Kilomita 105 na kupitia Miradi Mitano ya maendeleo, yenye thamani ya Sh.bilioni 4.9.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kahama Festo Kiswaga ametaja Miradi hiyo Mitano ya Maendeleo ambayo imepitiwa na Mwenge huo wa Uhuru, kuwa ni uzinduzi wa Mradi wa Maji, kuweka Mawe ya Msingi katika jengo la uchunguzi la magonjwa,mradi wa Taka Ngumu, pamoja na Bweni la watoto wenye ulemavu katika Shule ya Msingi Mwime.

Aidha, Mwenge huo wa Uhuru kesho utakimbizwa katika Halmashauri ya Ushetu na baada ya hapo utakabidhiwa katika Mkoa wa Tabora.

Kauli Mbiu ya Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka huu (2022) inasema "Sensa ni Msingi wa Mipango ya Maendeleo, Shiriki kuhesabiwa kwa Maendeleo ya Taifa.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka (2022) Sahili Nyanzabara Geraruma akizungumza kwenye uzinduzi na uwekaji mawe ya msingi kwenye miradi ya Maendeleo Manispaa ya Kahama.

Mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga, akizungumza kwenye Mbio za Mwenge wa Uhuru Manispaa ya Kahama.

Mbunge wa Jimbo la Kahama Jumanne Kishimba akizungumza kwenye Mbio za Mwenge wa Uhuru Manispaa ya Kahama.

Katibu Mkuu wa Habari, Tamaduni na Michezo kutoka Zanzibar Fatma Hamad Rajab akizungumza kwenye Mbio za Mwenge wa Uhuru Manispaa ya Kahama.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa (2022) Sahili Nyanzabara Geraruma akizindua Mradi wa Majisafi kutoka Ziwa Victoria wa Ngogwa-Kitwana Manispaa ya Kahama.

Kiongozi wa Mbio za Mwenye wa Uhuru kitaifa (2022) Sahili Nyanzabara Geraruma akikagua ujenzi wa Jengo la uchunguzi la Magonjwa katika Hospitali ya Manispaa ya Kahama.

Kiongozi wa Mbio za Mwenye wa Uhuru kitaifa (2022) Sahili Nyanzabara Geraruma, akikata utepe kabla ya kuweka Jiwe la Msingi katika Hospitali ya Manispaa ya Kahama.

Kiongozi wa Mbio za Mwenye wa Uhuru kitaifa (2022) Sahili Nyanzabara Geraruma, akiweka Jiwe la Msingi katika Jengo la uchunguzi la Magonjwa katika Hospitali ya Manispaa ya Kahama.

Muonekano wa Jengo la uchunguzi la Magonjwa katika Hospitali ya Manispaa ya Kahama pale litakapokamilika kujengwa.

Kiongozi wa Mbio za Mwenye wa Uhuru kitaifa (2022) Sahili Nyanzabara Geraruma, akikagua magari mapya mawili ya wagonjwa wa dharura katika Hospitali ya Manispaa ya Kahama ambayo yametokana na fedha za mapato ya ndani.

Muonekano wa Magari mawili ya wagonjwa wa dharura katika Hospital ya Manispaa ya Kahama.

Kiongozi wa Mbio za Mwenye wa Uhuru kitaifa (2022) Sahili Nyanzabara Geraruma, akikata utepe na kuweka Jiwe la Msingi katika Karakana ya utengezaji Aluminium na Samani katika eneo uwekezaji Viwanda la Ummy Mwalimu Manispaa ya Kahama.

Muonekano wa Karakana ya utengenezaji Aluminum na Samani ambayo imewekewa Jiwe la Msingi.

Kiongozi wa Mbio za Mwenye wa Uhuru kitaifa (2022) Sahili Nyanzabara Geraruma, akikagua na kuona kiwanda cha uchakataji Taka Ngumu cha Sindano Wiliamu Mchimu.

Ziara katika kiwanda cha Uchakataji Taka Ngumu ikiendelea.

Kiongozi wa Mbio za Mwenye wa Uhuru kitaifa (2022) Sahili Nyanzabara Geraruma, akikagua ujenzi wa Bweni la Wavulana wenye ulemavu katika Shule ya Msingi Jumuishi ya Mwime Manispaa ya Kahama.


Ukaguzi wa Bweni ukiendelea.

Kiongozi wa Mbio za Mwenye wa Uhuru kitaifa (2022) Sahili Nyanzabara Geraruma, akikata Utepe na kuweka Jiwe la Msingi katika Ujenzi wa Bweni la Wavulana Wenye ulemavu katika Shule ya Msingi Jumuishi ya Mwime.

Muonekano wa Bweni hilo.

Kiongozi wa Mbio za Mwenye wa Uhuru kitaifa (2022) Sahili Nyanzabara Geraruma, (kulia) wakitetea Jambo na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama Anderson Msumba.

Awali Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kahama Clemence Mkusa (kushoto) akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Msalala Solomoni Zedekia kwa ajili ya kuanza kukimbizwa katika Manispaa hiyo na kuipitia miradi Mitano ya Maendeleo.

Mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga akiushika Mwenge wa Uhuru.

Mbunge wa Jimbo la Kahama Jumanne Kishimba akiushika Mwenge wa Uhuru.

Mbunge wa Vitimaalum Santiel Kirumba akiushika Mwenge wa Uhuru.

Mbunge wa Vitimaalum Christina Mzava, akiushika Mwenge wa Uhuru.

Awali Mwenge wa Uhuru ukiwasili Manispaa ya Kahama kutokea Halmashauri ya Msalala.

Awali Mwenge wa Uhuru ukiwasili Manispaa ya Kahama kutokea Halmashauri ya Msalala.

Post a Comment

0 Comments