Header Ads Widget

SHINYANGA KUTUNGA SHERIA NDOGO KUTOKOMEZA NDOA ZA UTOTONI


Katibu Tawala msaidizi Mkoa wa Shinyanga Simbani Liganga, akizungumza kwenye kikao hicho.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

Mkoa wa Shinyanga umeanza mchakato wa kuandaa muongozo ambao utatumika kutunga sheria ndogo, kwa kufanya tathimini ya ndoa kabla haijafungwa pamoja na kujaza fomu, ili kujiridhisha ndoa hiyo kama inafungwa na watu wazima kwa lengo la kuzuia ndoa za utotoni.

Mratibu wa mpango mkakati wakutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto mkoani Shinyanga Tedson Ngwale, amebainisha hayo leo kwenye kikao cha kujadili muongozo wa utungwaji wa sheria ndogo kuanzia ngazi za chini, ambazo zitasaidia kutokomeza tatizo la ndoa za utotoni, pamoja na uzinduzi wa mradi wa unaolenga kuboresha afya na ustawi wavijana rika balehe, ambao utatekelezwa na Shirika la Doctors with Africa wilayani Shinyanga na Manispaa.

Ngwale amesema katika mpango mkakati wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto wa Mkoa huo Shinyanga (RSP 2020-2025), kuna kipengele kinazungumzia utungwaji wa sheria ndogo ili kutokomeza tatizo la ndoa za utotoni, ndiyo maana wameanza mchakato wa kuandaa muongozo ambao utasaidia kutunga sheria hiyo na kudhibiti ufungwaji wa ndoa za utotoni.

“Utungwaji wa sheria hizi ndogo utatusaidia kudhibiti tatizo la ndoa za utotoni, sababu kabla ya ufungwaji ndoa kutakuwa na fomu ya kujaza ambayo itakuwa kwenye Ofisi za watendaji, na kabla ya kufungwa ndoa kutakuwa na tathimini ya kujiridhisha kama ndoa hiyo hafungishwi mtoto,”Amesema Ngwale.

“Tunataka hadi kufikia mwaka 2025 ndoa za utotoni mkoani Shinyanga zisiwepo kabisa na kubaki kuwa historia,”Ameongeza.


Naye Katibu Tawala msaidizi Mkoa wa Shinyanga Simbani Liganga, amesema kufanya tathimini ya ndoa kabla ya kufungwa utasaidia kwa kiasi kikubwa kutokomeza ndoa za utotoni ambazo hukiuka haki za watoto kwa mujibu wa sheria namba 21 ya mtoto ya mwaka 2009 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2019 na sera ya mtoto ya mwaka 2008.

Aidha, akizungumzia mradi wa Shirika la Doctors with Africa ambao unalenga kuboresha afya na ustawi wa vijana wa rika balehe ,wenye lengo la kuimarisha mfumo wa afya kwa kuzingatia agenda ya kitaifa ya uwekezaji katika afya na maendeleo kwa vijana balehe, kuwa anaimani mradi huo utakuwa ni sehemu ya kudhibiti maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi VVU yanatotokana na ukatili wa kingono.

“Mradi huu ni mzuri sababu umekuja muda muafaka, sababu kuendelea kutokea vitendo vya ulawiti na ubakaji kwa vijana kuna sababisha kuenea kwa maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi VVU, Magonjwa ya zinaa, na kansa ya shingo ya kizazi,"Amesema Liganga.

Katika hatua nyingine amewataka wazazi mkoani Shinyanga kutowaachia jukumu la malezi wafanyakazi wa ndani, ndugu, marafiki, majirani na walimu, ili kutosababisha mmomonyoko wa maadili kwa watoto wao na kufanyiana ama kufanyiwa vitendo vya ukatili ambavyo huwa athiri kisaikolojia, kimwili na kiafya.

Amewataka wazazi pia wawe na tabia ya kukagua miili watoto wao, na wanapogundua wamefanyiwa vitendo vya ukatili wachukue hatua na siyo kufumbia macho vitendo hivyo kwa lengo la kulinda mahusiano na wakati vina athiri watoto na hata kupata maambukizi ya VVU.

Liganga amewapongeza pia wadau wa maendeleo mkoani humo kwa kazi kubwa ambayo wanaifanya katika mapambano dhidi ya mtukio ya ukatili kwa wanawake na watoto likiwamo na Shirika la UNFPA ambalo ndilo limefadhili kikao hicho, Shirika la ICS kwa kuunga juhudi za upatikanaji wa mpango mkakati wa Serikali, pamoja na mfuko wa Ruzuku wa wanawake (WTF-Trust) kuendeleza mapambano ya kupiga ukatili wa wanawake na watoto kwa kutoa ufadhili kwenye mashirika, na kuahidi Serikali kuendelea kuwapa ushirikiano.

Katibu Tawala msaidizi Mkoa wa Shinyanga Simbani Liganga, akizungumza kwenye kikao hicho.

Mratibu wa mpango mkakati wa Mkoa wa Shinyanga wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (RSP-VAWC 2020-2025) Tedson Ngwale akizungumza kwenye kikao hicho.

Mratibu wa mpango mkakati wa Mkoa wa Shinyanga wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto (RSP-VAWC 2020-2025) Tedson Ngwale akizungumza kwenye kikao hicho.

Meneja mradi wa CUAMM kutoka Shirika la Doctors with Africa Chiara Didone akizunguma kwenye kikao hicho.

Mwenyekiti wa huduma msaada wa kisheria John Shija akiwasilisha mada namna ya kutengeneza sheria ndogo.

Wajumbe wakiwa kwenye kikao.

Wajumbe wakiwa kwenye kikao.

Wajumbe wakiwa kwenye kikao.

Wajumbe wakiwa kwenye kikao.

Wajumbe wakiwa kwenye kikao.

Wajumbe wakiwa kwenye kikao.

Wajumbe wakiwa kwenye kikao.

Wajumbe wakiwa kwenye kikao.

Wajumbe wakiwa kwenye kikao.

Wajumbe wakiwa kwenye kikao.

Wajumbe wakiwa kwenye kikao.

Wajumbe wakiwa kwenye kikao.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA.

Post a Comment

0 Comments