Header Ads Widget

RAIS SAMIA AITISHA KIKAO CHA DHARURA KUJADILI TATIZO LA KUPANDA BEI YA MAFUTA NCHINI

Rais Samia Suluhu Hassan amewaagiza mawazi, makatibu wakuu wa baadhi ya Wizara kutafuta suluhisho la haraka la kukabiliana na tatizo la kupanda bei ya mafuta nchini.

Mkuu huyo wa nchi ametoa agizo hilo baada ya kuitisha kikao cha dharura kilichofanyika usiku wa kuamkia leo Mei 9, 2022 Ikulu ya Dar es Salaam cha kujadili tatizo la kupanda kwa bei ya mafuta ya ptroli, dizeli na mafuta ya taa nchini.

Miongoni mwa waliohudhuria katika kikao hicho ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Nishati January Makamba, Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba, makatibu wakuu wa wizara hizo na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato ya Tanzania (TRA) Alphayo Kidata.
 
SOMA ZAIDI HAPA; CHANZO MWANANCHI.

Post a Comment

0 Comments