Header Ads Widget

POLISI WATEKETEZA MASHAMBA YA BANGI

Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha limefanikiwa kuteteketeza Ekari nne na nusu za bangi katika eneo la Kisimiri juu, katika Halmashauri ya Wilaya ya Arumeru Mkoa wa Arusha.

Mkuu wa Operesheni za Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha, Gaudianus Kamugisha, amesema May 21,2022 wameteketeza bangi yote iliyokuwa shambani na nyumbani ambayo ni kiasi cha gunia 10 pamoja na debe moja la mbegu ya bangi kwa kushirikiana na Viongozi wa Serikali ya Vijiji.

Amesema operesheni hiyo ni mwendelezo wa operesheni zinazofanyika mara kwa mara katika Mkoa wa Arusha kwa ajili ya kupambana na kilimo cha bangi pamoja na Watumaji wa bangi.
 
SOMA HAPA ZAIDI CHANZO millardAyo.

Post a Comment

0 Comments