Header Ads Widget

BENKI YA EQUITY YAZINDUA TAWI KAHAMA


Katibu tawala wa wilaya ya Kahama , Timothy Ndanya katikati akifungua rasmi tawi la Benki ya EQUITY tawi la Kahama kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa taifa wa benki ya EQUITY ,Betty Kwoko na kulia ni meneja wa tawi hilo Beatus Tesha , picha zote na Patrick Mabula. Picha  na Patrick Mabula.
Meneja wa benki ya EQUITY tawi la wilaya ya Kahama, Beatus Tesha wa kwanza kushoto akieleza namna walivyojipanga kutoa huduma kwa wateja baada ya ufunguzi rasmi wa tawi la benki hiyo wilayani Kahama wa pili ni mgeni rasmi katika ufunguzi huo Timothy Ndanya na wa tatu kutoka kushoto ni Kaimu mkurugenzi wa taifa wa benki hiyo Betty Kwoko.
Mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa tawi la Benki ya EQUITY tawi la Kahama, Katibu tawala wa wilaya ya Kahama , Timothy Ndanya akitoa hutuba yake kwenye ufunguzi wa tawi la benki hiyo mjini Kahama .
Meneja wa tawi la benki ya EQUITY la wilaya ya Kahama Beatus Tesha akiongea wakati wa ufunguzi wa benki hiyo wilayani Kahama.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taifa wa benki ya EQUITY , Betty Kwoko akitoa hutuba wakati wa ufunguzi wa tawi la benki hiyo wilayani Kahama.
Wageni mbalimbali wakiwa kwenye ufunguzi wa benki ya EQUITY Tawi la wilaya ya Kahama .
Wafanyakazi wa benki ya EQUITY wakiwa na mgeni rasmi katibu tawala wa wilaya ya Kahama ,Timothy Ndanya aliyesimama katikati baada ya kufungua rasmi tawi la benki hiyo wilayani Kahama. Picha  na Patrick Mabula.

Na Patrick Mabula , Kahama.

Serikali wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga imetoa ushauri wakulima , wajasiriamali wadogo ,wa kati na wakubwa kuchangamkia fursa za uwekezaji unaofanywa na taasisi za fedha wilayani Kahama ziweze kuwanufaisha kiuchumi na kujiletea maendeleo.


Ushuari huo umetolewa leo Mei 25,2022 na Katibu Tawala wa wilaya ya Kahama , Timothy Ndanya kwenye uzinduzi rasmi wa Benki ya EQUITY tawi la Kahama na kuwataka wananchi  kuchangamkia fursa mbalimbali za kiuchumi zinazotolewa na taasisi za fedha , mabenki katika kujiletea maendeleo.


Ndanya amesema wilaya ya Kahama ina bahati ya kuwepo na taasisi nyingi za kifedha kwa kuwa na matawi 12 ya benki yaliyofunguliwa katika wilaya ya Kahama na yamekuwa yakitoa fursa mbalimbali za kiuchumi na kuwataka kuzitumia ziweze kuwasaidia kukuza mitaji yao na kujiletea maendeleo.


Awali katika hotuba yake Kaimu mkurugenzi mtendaji wa EQUITY benki Tanzania, Betty Kwoko amesema benki yao ni biashara katika malengo yake , lengo lake kuu ni kuboresha maisha ya kila Mtanzania kiuchumi na jamii.


Kwoko amesema benki ya EQUITY ni miongoni mwa taasisi bora ya fedha katika kutoa huduma bora kwa wateja wake na kwa wafanyabiashara wadogo , wa kati na wakubwa na kutokana na utafiti wake wilaya ya Kahama yenye halmashauri tatu inamalengo ya kibiashara katika kukuza uchumi wa wananchi wake.


Amesema katika mpango wa mkakati wa Benki ya EQUITY wa miaka mitano wameweka malengo sawa na ya serikali ya wilaya ya Kahama kuhusu biashara ya Madini ya dhahabu , Almasi na kwa upande wa kilimo cha mazao ya Pamba , Tumbaku , Alizeti , Choroko , Degu kuhakikisha wanawasaidia kiuchumi wanaofanya shughuli hizo.

Kwoko amesema katika mpango huo pia wamejumuisha pamoja na wajasiriamali wadogo , wa kati na wakubwa wamewajumisha kwenye vipaumbele vya benki hiyo na kuwataka wananchi kuchangamkia huduma mbalimbali zitakazotolewa pamoja na fursa ya kupata elimu bule ya fedha na uwekezaji wa amana , utunzaji wa fedha na mikopo nafuu kwa ujasiriamali mdogo , wa kati na mkubwa.


Nao wananchi na wateja waliofika kwenye uzinduzi huo John Manjale na Delfine Kalunde walipongeza mpango mkakati wa benki hiyo katika kuwasaidia watu wa kada zote za kiuchumi ziweze kuwasaidia kubadilisha maisha na kujiletea maendeleo.

Post a Comment

0 Comments