Header Ads Widget

MAKONDA AITWA POLISI

Kamanda Muliro amtaka Makonda kuripoti polisi

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amemshauri Paul Makonda kwenda kituo cha Polisi kuripoti tuhuma alizozitoa mtandaoni, ikiwamo ya kudai kutishiwa maisha.


“Sijaongea naye (Makonda), lakini kupitia ninyi (vyombo vya habari), namshauri aende kituo chochote cha polisi endapo madai aliyoyatoa yana ukweli. Inategemea yeye (Makonda) anakaa wapi, lakini aende kituo cha polisi cha karibu kwa ajili ya kutoa maelezo ya madai yake,” alisema Muliro.

SOMA HAPA ZAIDI CHANZO MWANANCHI.

Post a Comment

0 Comments