Header Ads Widget

DC MBONEKO AKABIDHI BASI DOGO AINA YA TATA KIKUNDI CHA VIJANA MKOPO WA HALMASHAURI KUONDOA TATIZO LA USAFIRI KWA WANAFUNZI

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akiendesha Basi dogo aina ya TATA la kikundi cha Vijana na Mapambano, ambalo amelikabidhi kwao kupitia Mkopo wa Asilimia 10 wa Halmashauri Manispaa ya Shinyanga, ambapo Asilimia Nne hutolewa kwa vijana na wanawake, na Asilimia mbili hutolewa kwa watu wenye ulemavu.

Muonekano wa Basi dogo aina ya TATA ambalo wamekabidhiwa kikundi cha vijana na Mapambano kupitia Mkopo wa Asilimia 10 wa Halmashauri ambapo asilimia Nne hutolewa kwa vijana na wanawake na Asilimia Mbili kwa watu wenye ulemavu.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA.

MKUU wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, amekabidhi Basi dogo aina ya TATA kwa kikundi cha vijana na mapambano Manispaa ya Shinyanga, ambalo litakuwa likitumika kubeba wanafunzi kwa ajili ya kuwapeleka shule, na baadae kubeba abiria na saa 10 alasiri kuwarudia wanafunzi majumbani hadi saa 12 jioni, kisha kuendelea na ubebaji wa abiria.


Zoezi la kukabidhi Basi hilo limefanyika leo katika eneo la Manispaa ya Shinyanga, na kushuhudiwa na Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa Baraka Shemahonge, baadhi ya wananchi na watumishi wa Halmashauri hiyo ya Manispaa ya Shinyanga.

Mboneko akizungumza wakati wa kiukabidhi basi hilo, amewataka vijana hao walitunze pamoja pesa ambazo wanazipata wazifanyie maendeleo na ikiwezekana waongeza basi jingine na kuinuka kiuchumi.

“Rais wetu Samia Suluhu Hassani alisema mikopo hii asilimia 10 ya Halmashauri ifanyiwe vitu vikubwa kwa kuonekana miradi yenye tija, na leo Manispaa ya Shinyanga tunakabidhi Basi katika kikundi cha vijana, pamoja na Mashine ya kutotoreshea vifaranga vya kuku kwa kikundi cha wanawake,”alisema Mboneko.

“Wanafunzi wetu walikuwa wakipata shida sana ya usafiri kwenda shule, na mimi nilipiga marufuku kupewa lifti bali wavulie sababu Serikali tutalifanyia ufumbuzi tatizo hilo, na leo tumekabidhi vijana Basi kwa ajili ya kuwapeleka shule na kuwarudisha,”aliongeza.

Aidha, alitoa onyo pia kwa wanafunzi wasije wakachorachora Basi hilo pamoja na kuharibu viti, bali wawe wastarabu ili waendele kunufaika na matunda ya Serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassani, huku akiwasihi wasome kwa bidii na kusiwepo Ziro hata moja kwenye mitihani yao.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa wilaya, alitoa maekelezo ya Nauli kuwa Basi hilo litakuwa likibeba wanafunzi kwa Sh,200 na watu wazima Sh.500.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura, alisema Manispaa hiyo ina mpango wa kutoa Mabasi mengine Manne kwa ajili ya kazi hiyo ya kubeba wanafunzi na baadae abiria wa kawaida.

Naye Afisa Maendeleo ya jamii Manispaa ya Shinyanga John Tesha, alisema kikundi kicho cha vijana walikikopesha Sh. milioni 60 kwa ajili ya kununua Basi hilo, ambapo kiasi kingine cha fedha walikiongeza wao wenyewe, huku akibainisha kwa upande wa mashine ya kisasa ya kutotoresha vifaranga vya kuku wameinunua kwa Sh. milioni 2.2.

Aidha alisema Halmashauri hiyo imeendelea kutoa mikopo ya asilimia 10 kwa vikundi vya vijana, wanawake, na watu wenye ulemavu, kuwa kwa kipindi cha kuanzia Julai hadi Disemba (2021-2022) kuwa kimetolewa kiasi cha fedha Sh.milioni 175.0

Alifafanua kuwa fedha hizo za mkopo zimetolewa kwa mchanganuo ufuatao, ambapo vikundi vitano vya wanawake vimepatiawa Sh. milioni 46, Vijana vikundi Vinne Milioni 126, kikundi kimoja cha watu wenye ulemavu Sh.milioni 3.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kikundi cha Mapambano ambao wamekabidhiwa Basi hilo Jasamila Maduhu, ameipongeza Serikali kwa kuwapatua mkono huo wa Basi ambalo litabadili maisha ya kiuchumu na kubainisha kuwa wamelinunua kwa bei ya Sh, milioni 105.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza wakati wa zoezi hilo la kukabidhi Basi dogo aina ya TATA na Mashine ya kutotoresha vifaranga vya kuku.

Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko, akizungumza wakati wa zoezi hilo la kukabidhi Basi dogo na Mashine ya kutotoresha vifaranga vya kuku.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Jomaary Satura, akizungumza kwenye zoezi hilo la kukabidhi Basi dogo na Mashine ya kutotoresha vifaranga vya kuku.

 

Afisa Maendeleo ya jamii Manispaa ya Shinyanga John Tesha, akisoma taarifa ya utoaji mikopo kwa vikundi vya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu.

Mwenyekiti wa kikundi cha vijana na Mapambano Jasamila Maduhu, akiishukuru Serikali kwa kuwapatia mkopo huo wa Basi dogo aina ya TATA.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akiendesha Basi hilo dogo aina ya TATA  la kikundi cha Vijana na Mapambano, ambalo amelikabidhi kwao kupitia Mkopo wa Asilimia 10 wa Halmashauri Manispaa ya Shinyanga, ambapo Asilimia Nne hutolewa kwa vijana na wanawake na Asilimia mbili hutolewa kwa watu wenye ulemavu.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akiendesha Basi hilo aina ya TATA.

  Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko akiwa ndani ya Basi hilo la aina ya TATA.

Watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga wakiongozwa na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Jomaary Satura (kushoto) wakiwa ndani ya Basi hilo aina ya TATA.

Watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga wakiwa ndani ya Basi aina ya TATA.

Watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga wakiwa ndani ya Basi aina ya TATA.

Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa Baraka Shemahonge (kushoto) akiwa ndani ya Basi aina ya TATA.

Mwenyekiti wa kikundi cha vijana na Mapambano Jasamila Maduhu, akiwa amesimama kwenye Basi dogo aina ya TATA ambalo wamepewa na Halmashauri kupitia Mkopo wa vijana.

Muonekano wa Basi dogo aina ya TATA ambalo wamekabidhiwa kikundi cha vijana na Mapambano kupitia Mkopo wa Asilimia 10 wa Halmashauri ambapo asilimia Nne hutolewa kwa vijana na wanawake na Asilimia Mbili kwa watu wenye ulemavu.

  Picha ya pamoja ikipigwa mara baada ya zoezi hilo la kukabidhi Basi dogo aina ya TATA kwa kikundi cha vijana na mapambano kumalizika.

 

Picha za pamoja zikiendelea kupigwa.

 

Picha za pamoja zikiendelea kupigwa.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akikabidhi Mashine ya kisasa ya kutotoresha vifaranga vya kuku (Incubator) kwa kikundi kingine. Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akikagua mashine hiyo ya kutotoresha vifaranga vya kuku.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA.

Post a Comment

0 Comments