Header Ads Widget

CHAMA KIKUU CHA USHIRIKA WILAYANI KAHAMA(KACU) KIMEFANYA UCHAGUZI NA KUPATA UONGOZI MPYA


 CHAMA KIKUU CHA USHIRIKA WILAYANI KAHAMA(KACU) KIMEFANYA UCHAGUZI NA KUPATA UONGOZI MPYA.

Mrajisi msaidizi kutoka makao makuu Dodoma Emanuel Sanka ambaye alikuwa msimamizi wa uchaguzi huo kutoka kushoto ni katibu tawala wilaya ya Kahama Timothy Ndanya na  kulia kwake ni mrajisi wa vyama vya ushirika mkoa Hilda Boniface.

 Wajumbe wa mkutano maalum kutoka vyama mbalimbali vya msingi wakisubiri maelekezo ya kupiga kura

 

Wagombea nafasi ya uenyekiti wa chama kikuu cha ushirika wilayani Kahama mkoani Shinyanga KACU ambapo upande wa kwanza kulia ni Emanuel Nyambi na Hamisi Majogaolo.

 


      Mwenyekiti wa KACU ,Hamis Majogolo aliyesimama akiongea baada ya kupata ushindi.

 Na Neema Sawaka

Kahama

CHAMA kikuu cha ushirika wilayani Kahama  mkoani Shinyanga (KACU) kimefanya  uchaguzi na kumpata mwenyekiti Hamis Majogolo na makamu mwenyekiti Tano Nsabi kwa kuongoza kwa kipindi cha  miaka miwili iliyobaki.

Mrajisi msaidizi wa vyama vya ushirika kutoka makao makuu Dodoma Emanuel Sanka  alikuwa msimamizi wa uchaguzi huo uliofanyika  jana na  viongozi hao kutangazwa washindi  baada ya kupigiwa kura na wajumbe 245 waliohudhuria mkutano maalum kwaajili ya uchaguzi.

Sanka alimtangaza mwenyekiti mpya wa ushirika  huo Hamis Majogolo  kwa kupata kura 127  na kumzidi mshindani wake Emanuel Nyambi aliyepata kura 117 huku kura moja ikiwa imeharibika.

Sanka pia alimtangaza  makamu mwenyekiti  Tano Nsabi  aliyepata kura 137 baada ya kuwashinda wapinzani wenzake watatu waliokuwa  kwenye kinyang’anyiro hicho huku mwakilishi  wa  vyama vya msingi taifa  Daniel Mwita aliyepata kura 102 akitangazwa mshindi kwa kuwazidi wapinzani wenzake wanne  katika kinyang’anyiro hicho.

“Kwa mujibu wa sheria na  katiba ya  ushirika  viongozi hao watadumu kwa miaka miwili baada ya miaka mitatu  baada ya uchaguzi  huo kufanyika mwaka  jana mwanzoni  na viongozi  waliochaguliwa  kuondoka na mwingine kufariki”alisema  Sanka.

Mrajisi wa  vyama vya ushirika mkoa wa Shinyanga Hilda Boniface alisema kuwa  maamuzi waliyoyatoa wajumbe kupata viongozi watayazingatia  na kuyaheshimu  huku akiwataka wajumbe kumpatia ushirikiano wakutosha mwenyekiti ili kufanya ushirika huo kusonga mbele zaidi.

 Katibu tawala wilaya ya Kahama Timothy  akiwa mgeni rasmi katika uchaguzi huo kwa niaba ya mkuu wa wilaya hiyo Festo Kiswaga alisema kuwa viongozi  waliochaguliwa wajue wamebeba maisha ya wananchi walioko kwenye maeneo yao  kuanzia sasa makundi yaliyokuwepo yavunjwe kazi iendelee.

“Kweli  viongozi mmepata tunataka kuona mafanikio yakutosha katika usimamizi wa mazao ya pamba na tumbaku kwa wakulima kwani mafanikio tumeyaona kupitia ushirika msimu uliopita mmeweza kununua pamba kilo moja sh 1500 ndiyo serikali inataka uongozi imara unaowaletea faida  wakulima”alisema Ndanya.

Mwenyekiti aliyechaguliwa  Hamis Majogolo alishukuru wajumbe kumchagua na kumuamini kwani ameziona changamoto zilizopo kwa wakulima wa zao la pamba na tumbaku atahakikisha anatembelea kila amcos kwa kushirikiana na wataalamu ili kuweza kuwanyanyua wakulima  waendane na soko.

Uchaguzi huo umekuja kufuatiwa na aliyekuwa mwenyekiti wa  ushirika huo Emanuel Cherehani kuchaguliwa mwaka jana kuwa mbunge wa jimbo la Ushetu  na sheria kumtaka kuachia nafasi hiyo huku makamu mwenyekiti Geofrey Mbuto  aliyefariki dunia mwezi Janurai mwaka huu.

Post a Comment

0 Comments