Header Ads Widget

MGODI HAUHUSIKI NA UCHAFUZI WA MAJI YA MTO MARA


Meneja Mkuu wa Mgodi wa Dhahabu wa Barrick North Mara, Apolinary Lyambiko akielezea jambo kwa waandishi wa habari waliotembelea mgodi huo uliopo Wilaya ya Tarime mkoani Mara karibuni wakati wa kampuni hiyo ilipotangaza kufikia lengo lao la kukamilika kwa mradi wa kuhifadhi maji yatokanayo na uchenjuaji wa dhahabu pamoja na kusimika mitambo ya kisasa ya kusafisha maji
Mgodi wa Dhahabu wa North Mara, umepata taarifa za tuhuma zinayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu utiririshaji wa zebaki kwenye Mto Mara.

North Mara imebainisha mbali na eneo husika kuwa umbali wa kilomita 80-85 chini ya mgodi, zebaki si sehemu ya orodha ya vitendanishi vya mgodi huo wala haitokei kiasili katika eneo hilo na hivyo basi, kama kuna zebaki yoyote iliyopatikana katika mto haiwezi kuhusishwa na mgodi.

Meneja wa Barrick nchini,Georgia Mutagahywa, amesema Mamlaka ya Bonde la Maji ya Ziwa Victoria mara kwa mara imekuwa kichukua sampuli za maji katika maeneo yaliyo jirani na migodi na mgodi wenyewe una mpango madhubuti wa ufuatiliaji wa maji ya ardhini na hakuna ushahidi wa kuwepo zebaki au uchafu mwingine wowote kwenye maji ndani au karibu na maeneo ya uzalishaji.

Aidha, Serikali ya Tanzania iliunda timu ya wataalamu inayoongozwa na Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) ambayo imekuwa ikifanya kazi kwa karibu na Mgodi wa Dhahabu wa North Mara ili kuhakikisha hakuna uchafuzi wa mazingira au maji unaotokea katika mgodi huo na katika maeneo yanayouzunguka.

Mgodi pia umefikia lengo muhimu la uhifadhi wa taka zitokanazo a mchakato wa uchenjuaji wa madini kwa kupunguza kiasi cha maji yaliyohifadhiwa kwa kiasi kikubwa kutoka mita za ujazo milioni 7 hadi mita za ujazo 800,000 ndani ya kipindi cha miaka miwili, kama ilivyokubaliwa katika Mkataba wa Maelewano na NEMC.

Haya ni mafanikio makubwa, ambayo yanaonyesha zaidi dhamira na jitihada za Mgodi wa Dhahabu wa North Mara zinakwenda sambamba kwa kuhakikisha hakuna uchafuzi wa maji au mazingira kwenye Mgodi na maeneo yanayouzunguka.


Post a Comment

0 Comments