Header Ads Widget

SERIKALI YA WILAYA YA KAHAMA YAKARIBISHA WAWEKEZAJI WANAWAKE SEKTA YA MADINI.

 SERIKALI YA WILAYA YA KAHAMA YAKARIBISHA WAWEKEZAJI WANAWAKE SEKTA YA MADINI.

 

Alfred Mwita mkemia wa mgodi wa dhahabu  wa  Canuck akielezea namna ya uchenjuaji  wa dhahabu unavyofanyika. 

 Na Neema Sawaka

 Serikali  wilayani kahama  inakaribisha  wawekezaji wanawake katika sekta ya  madini kwani maeneo ya uwekezaji  yapo na hawanabudi kuchangamkia fursa hiyo  ilii kukuza  mitaji  na kujikwamua kiuchumi.

Serikali imeweka mazingira rafiki ya uwekezaji katika sekta ya madini , ambapo zamani wanawake walikuwa wanabaguliwa kushiriki kwenye  uwekezaji kwenye rasilimali  madini.
 
 Hayo yalisemwa na Mkuu wa wilaya ya Kahama Festo Kiswaga alipotembelea mgodi wa Kati wa Canuck mining  company limited  uliopo katika Kijiji  Cha  numbi  katika kata  ya mwakata halmashauri ya Msalala  katika ziara yake ya  kukagua shughuli za maendeleo  wilayani humo.

Kwa sasa kuna baadhi ya wanawake  ambao tayari  wameingia  kwenye sekta ya madini  ambao tayari wanamiliki  maduara  na wengine wanajihusisha na uchimbaji.
Serikali imeweka mazingira wezeshi  kwa wanawake kushiriki kwenye shughuli za uchimbaji    madini na maeneo ya kuwekeza yapo  na leseni zinatolewa kwa wale wanaohitaji   kuwekeza kwenye sekta  hiyo ya madini.
 
Kiswaga alisema,ardhi  iliyopo kahama  ni ya mheshimiwa Rais  na  mwananchi. anayetaka    kushughulika na  madini na kuwekeza  anafika kwenye mamlaka husika  kwa ajili ya kufuata utaratibu wa kuwekeza  kwenye eneo alilolidhika nalo.

Kwa upande wake  Meneja    Rasilimali watu wa  mgodi  huo wa Canuck  David  Deogratius  alisemaa katika mgodi huo wameajili wafanyakazi 240 Kati yao 22 ni wanawake.

Katika idara mbali mbali ambapo  wanawake wana mchango    mkubwa katika sekta hiyo."|Mgodi umetoa ajira hizo 240 kwa wananchi waliokaribu na  wale wanaotoka katika vijiji vinavyozunguka  mgodi huo|".Alisema David
 
Meneja huyo alisema  shilingi milioni 10  zilitumika kulipa kifuta jasho  kwa wachimbaji wadogo walikokuwa wakichimba na kumiliki na Maduara kwenye eneo Hilo. Huku milioni 159  zilitumika kulipa fidia za  ardhi  na mazao. Pamoja na nyumba  kwa wananchi waliopisha uwekezaji huo.

Mmoja wa wachimbaji  wa mgodi huo Leah    makoye. Alisema kuwa    wanawake. Wengi    wamekuwa wakidhani    kazi za uchimbaji zinafanywa na wanaume tu. Jambo ambalo hata wanawake wanaweza kufanya shughuli za uchimbaji. Ambapo hata yeye ameajiriwa na kampuni hiyo kwa ajili ya shughuli za uchimbaji  na tayari anasomesha watoto kupitia kazi hiyo na   anamiliki nyumba  na rasilimali zingine kupitia kazi    za uchimbaji.
TUTUMIE HABARI,PICHA,MATUKIO AU TANGAZO LAKO TUKUWEKEE KWENYE SHINYANGA PRESS CLUB BLOG,WASILIANA NASI KWA Email : shinyapress@gmail.com Simu/WhatsApp 0756472807