Header Ads Widget

MKUU WA MKOA AFUTA LIKIZO KWA WATUMISHI

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya (RC), Juma Homera amefuta likizo kwa watumishi wote wa Serikali mkoa huo ambao idara zao zinahusika na ujenzi wa miradi ya miundombinu ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na madawati ambapo tayari Serikali imetoa fedha za miradi hiyo.

Homera ametoa agizo hilo leo Jumanne Desemba 7, 2021 wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Mwakibete alipotembelea chanzo cha maji cha Nzovwe kinachosimamiwa na Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira (Mbeya-Uwwas) huku akibainisha kufuta likizo kwa wakuu wa Wilaya, wakurugenzi wa halmashauri zote, maofisa manunuzi, watendaji wa kata, wahasibu na watendaji wa idara zingine za Serikali.

SOMA ZAIDI HAPA CHANZO MWANANCHI


Post a Comment

0 Comments