Header Ads Widget

JESHI LA POLISI SHINYANGA LANYOOSHEWA KIDOLE NA BAADHI YA ASASI ZA KIRAIA,RPC KYANDO AWAITA OFISINI.

Washiriki kutoka baadhi ya asasi za Kiraia zinazoshughulika na mradi wa kupinga mimba na ndoa za utotoni wakiwa wanafuatilia uwasilishwaji wa mradi ulivyotekelezwa kwa kila shirika.
Katibu wa kamati ya Ulinzi na Usalama wa  Wanawake na Watoto ya Mkoa wa Shinyanga Bw. Thedson Ngwale ambaye pia ni Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Shinyanga, akizungumza kwenye kikao cha Asasi za kiraia za Mkoa wa Shinyanga zinazoshughulika na mradi ya kupinga Mimba na Ndoa za Utotoni.
===============

Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga limeshauriwa kufikiria madhara ya kudumu yanayompata mhanga wa ukatili wa kijinsia ambapo limelaumiwa kwa kuwa sehemu ya kukwamisha mapambano ya ukatili  kwa kutokukutoa ushirikiano dhidi ya matukio ya ukatili kwa watoto hayataisha.

Katibu wa kamati ya ulinzi na usalama wa  Wanawake na Watoto ya Mkoa wa Shinyanga Bw. Thedson Ngwale amesema hayo  kwenye kikao cha asasi za kiraia zilizokuwa zimefadhiliwa na shirika la Firelight Foundation la nchini Marekani ambacho kimefanyika kuanzia 03 November hadi 05 November 2021.

Amesema baadhi ya matukio yanashindwa kufanyiwa kazi kwa wakati na wananchi kuripoti matukio mengi lakini yanayofanyiwa kazi ni machache hiyo ni kwa sababu sheria ya ushahidi inaruhusu kesi kama hizo za jinai lakini zina dhamana,hivyo mtu akipata dhamana anaenda kwenye mahakama ya familia kati ya familia ya mhanga na  mtuhumiwa kwa mantiki hiyo wanaenda kumtengeneza mhanga afiche ukweli kwa kuahidiwa au kupewa kitu na familia ya mtuhumiwa.

Ngwale ambaye pia ni Afisa maendeleo ya jamii Mkoa wa Shinyanga pia amewaomba viongozi wengine wa ngazi ya Taifa kwamba kuna sheria zinahitaji mabadiliko na kesi zisiondolewe mahakamani kama ushahidi haueleweki ili mkemia mkuu wa Serikali athibitishe kupitia vipimo vya Vina saba(DNA) baada ya mtoto kuzaliwa ili kugundua mthumiwa ni yupi ili huo mchezo wa kupikwa kwa ushaidi ukome.

Mmoja wa washiriki wa kikao hicho Mkurugenzi  wa shirika la Agape Aids Control Program Bw.John Myola  amemwomba Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga atengeneze utaratibu kuawapata askari wa dawati la Jinsia weye maadili na  wasikae zaidi  ya miezi sita bali angalau miezi mitatu halafu wawekwe wengine kwa sababu kesi za ukatili zinazowafikia wanazigeuza kuwa fursa kwa kuwa kuna mazingira ya rushwa na kuharibu kesi za mimba na ndoa za utotoni.

 Akitolea mfano wa kesi ambayo walienda mkamata baba mtu mzima aliyekutwa na binti wa miaka 14  wa darasa la tano mwenye mimba ya miezi mitano na humo ndani alikuwa na mdogo wake mwenye umri wa miaka tisa ambapo mtoto huyo ni mtoto wake wa Kambo maana yake Mama mzazi wa huyo mtoto ameolewa na huyo baba na wakati wameenda kumkamata mama yake alikuwa amesafiri kwa muda wa miezi miwili maana yake huyo baba alikuwa anamtumia mama na mtoto kama wake zake.

Ameendelea kueleza kuwa mtuhumiwa huyo alikaa polisi wiki mbili bila kwenda mahakamani ingawa alikamatwa na vielelezo vyote,matokeo yake amepewa dhamana na baadae wanaambiwa mtuhumiwa ametoroka,hivyo ameshauri polisi waliopo dawati la jinsia wawe wanabadilishwa wasikae pale kimazoea kwani kwa kuna mazingira ya rushwa kutokana na kesi zinavyoyeyuka.

Amesema wao kama mashirika yanayopinga mimba na ndoa za utotoni wanavunjika moyo kutokana na vitendo vinavyofanywa na baadhi ya maafisa wa Jeshi la Polisi waliopo dawati la jinsia kutengeneza mazingira ya kupoteza ushahidi.

Kwa upande wake Afisa Miradi wa ulinzi na haki za watoto kutoka Firelight Foundation bi. Tomaida Banda amesema wao kama shirika walifanya utafiti wa mimba na ndoa za utotoni nchini Tanzania wakagundua kwamba Shinyanga ni mmoja wa mkoa unaokabiliwa na changamoto hiyo na yapo mashirika mengi yanahusika na kupinga vitendo hivyo ndipo wakaamua kuwa wafadhili kwa mashirika hayo takribani 12 ili kuwawezesha kupambana na janga hilo na amesema kwa kuwa mradi umeisha na wameukabidhi kwa Serikali,baada ya kikao cha tathmini watafanya utafiti mwingine ndipo waje kuwekeza tena.

Akijibu malalamiko yaliyotolewa na baadhi ya asasi hizo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP George Kyando amesema kama wana uthibitisho wa hizo tuhuma waende ofisini wazungumze na wampe taarifa zenye uthibitisho au viashiria vyovyote vyenye mianya ya rushwa ili achukue hatua kwa watakaobainika.

"Askari wetu ni weledi na wamepitia mafunzo, kama kuna tabia kama hizo na zimethibitika tutawachukulia hatua maana huenda siyo wote wapo safi katika kazi",amesema

Aidha mashirika yasiyokuwa ya kiserikali ya mkaoni Shinyanga yaliyokuwa yamefadhiliwa na shirika la Firelight Foundation kwa ajili ya kupinga mimba na ndoa za utotoni ni pamoja na OPE,AGAPE,WEADO,ICS,TVMC,MKOMBOZI,TAI,CHIDEPA,RAFIKI SDO,YWL NA PWWCO.

Katibu wa kamati ya ulinzi na usalama  wawanawake na watoto Mkoa wa Shinyanga Bw. Thedson Ngwale ambaye pia ni Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Shinyanga akizungumza kwenye kikao cha baadhi ya asasi za kiraia za Mkoa wa Shinyanga zinazoshughulika na miradi ya kupinga mimba na ndoa za utotoni.
Mkurugenzi wa Shirika la OPE Bw. William Shayo akizungumza kwenye kikao cha  asasi za kiraia za Mkoa wa Shinyanga zinazoshughulika na miradi ya kupinga mimba na ndoa za utotoni.
Mkurugenzi wa Shirika la TVMC Bw.Musa Ngangala akizungumza kwenye kikao cha asasi za kiraia za Mkoa wa Shinyanga zinazoshughulika na miradi ya kupinga mimba na ndoa za utotoni.
Afisa Maendeleo ya jamii halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Bw. Deus Muhoja akizungumza katka  kikao cha baadhi ya asasi za kiraia za mkoa wa shinyanga zinazoshughulika na miradi ya kupinga mimba na ndoa za utotoni.
Afisa Miradi wa ulinzi na haki za watoto kutoka Firelight Foundation Bi.Tomaida Banda akizungumza kwenye kikao cha baadhi ya asasi za kiraia za Mkoa wa Shinyanga zinazoshughulika na miradi ya kupinga mimba na ndoa za utotoni.

Washiriki wa kikao hicho cha baadhi ya asasi za kiraia zinazoshughulika na mradi wa kupinga mimba na ndoa za utotoni wakiwa katika picha pamoja 

Picha zote na Shinyanga Press blog

Post a Comment

0 Comments