Header Ads Widget

MWANAUME ANUSURIKA KIFO MADAI YA KUCHOMWA KISU KICHWANI, TUMBONI, NA MKEWAKE WIVU WA KIMAPENZIPicha ya Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga George Kyando

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MWANAUME Simon Robert (43) Mkazi wa Katunda Ibinzamata Manispaa ya Shinyanga, amenusurika kifo mara baada ya kuchomwa kisu na mkewake Amina Hamis (32), ambaye amedaiwa kumchoma kichwa,tumboni na kumsababishia majeraha.
 
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga George Kyando, akitoa taarifa ya tukio leo kwa vyombo vya habari, amesema limetokea usiku wa kuamkia leo majira ya saa 7, ambapo mwaume huyo alinusurika kifo mara baada ya kuchomwa kisu na mkewake.

Alisema chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi, ambapo wanandoa hao walianza kugombana, mara baada ya kutoaminiana kwenye mahusiano yao, ndipo mwanamke alipochukua kisu na kumchoma mwenzake kichwani na tumboni.

“Majeruhi amelazwa katika Hospitali ya Rufani mkoani Shinyanga akipatiwa matibabu, na hali yake ni mbaya sababu alichomwa kisu sehemu mbaya za kichwani na tumboni,”alisema Kyando.

Aidha, alisema Jeshi la Polisi limamshikilia mwanamke huyo kwa tuhuma za kumchoma mmewake na kisu, ambapo upelelezi ukikamilika atafikishwa mahakamani kujibu mashitaka yanayomkabili kwa mujibu wa sheria.

Katika hatua nyingine Kamanda alitoa wito kwa wanandoa wote, wajiepushe na masuala ya wivu wa kimapenzi, ambapo kama wana migogoro wakae wazungumze, na siyo kujichukulia sheria mkononi.

xxxxxxxxxxxx

Post a Comment

0 Comments