Wafanyakazi wa Tume ya Madini makao makuu wakiwa na vitu mbalimbali walivyowapelekea baadhi ya wafungwa katika gereza la Isanga jijini Dodoma
Na Mwandishi wetu, Dodoma
Leo tarehe 03 Machi, 2021 wanawake kutoka Tume Ya Madini Makao Makuu wametembelea gereza la wanawake la Isanga lililopo jijini Dodoma ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Wanawake Duniani.
Akizungumza kabla ya kuanza kwa ziara hiyo, Afisa Utawala wa Tume ya Madini, Joyce Rweyemamu amesema ni sehemu ya kugusa jamii hususan wanawake walioko magerezani ambao wamesahaulika.
"Wanawake wengi wamekuwa wakigusa jamii kwa namna mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwasaidia yatima,wajane na wagonjwa lakini sisi kama wanawake kutoka Tume ya Madini tumeamua kufanya kitu cha tofauti kwa kuwatembelea wanawake waliopo magerezani kama sehemu ya kuwatia moyo na kufahamu kuwa wanatengenezwa na kuwa bora mara baada ya kumaliza kutumikia adhabu ya kifungo", amesema Rweyemamu.
Katika hatua nyingine, Rweyemamu amewataka wanawake katika Taasisi nyingine na jamii kwa ujumla kuwa na moyo wa kugusa jamii kwa kuwasaidia watu wenye uhitaji.
Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani kwa mwaka 2021 ambayo kilele chake ni Machi 08, 2021 yanabebwa na kaulimbiu ya "Wanawake katika uongozi, chachu kufikia dunia yenye usawa"
0 Comments