Header Ads Widget

MZEE WA MIAKA 58 AFARIKI AKIFANYA NGONO 'LODGE', POLISI YACHUNGUZA CHANZO


 Mzee huyo wa miaka 58, alipatwa na mhudumu wa usafi akihema sana lojini - Alikimbizwa katika Hospitali ya JM Kariuki ambapo alithibitishwa kufariki - Wakati wa uchunguzi, kondomu ilipatikana kwenye sehemu zake nyeti 

Maafisa wa polisi katika kaunti ya Nyandarua wanachunguza hali iliyopelekea kifo cha mzee mmoja mwenye miaka 58, ambaye aliaga dunia baada ya kulala lojini. 

 Kulingana na ripoti ya polisi, Edith Wairimu Mwangi alimpata marehemu akihema sana baada ya kuenda kusafisha chumba hicho katika nyumba ya kulala wageni ya Heshima Lodge Olkalau. 

Kisha mwanamke huyo wa miaka 55, alikimbia katika Kituo cha Polisi cha Olkalau kupiga ripoti ambapo maafisa wa polisi walikimbia katika eneo la tukio wakiandamana pamoja na makachero kutoka Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI). 

Ambulensi ilitafutwa na alikimbizwa katika Hospitali ya JM Kariuki ambapo alithibitishwa kufariki. 

"Wakati mwili wake ulikuwa unakaguliwa, alipatikana na kondomu kwenye uume wake. Eneo la tukio lilichunguzwa na maafisa wa CSI kabla ya mwili huo kupelekwa mochari ukisubiri kufanyiwa upasuaji," ilisoma ripoti ya polisi. 

Mwanamume huyo pia alikuwa mlinzi wa lojini hiyo. 

Kisa hiki kinakujia siku chache baada ya mwanamume mwingine mwenye miaka 52, kuzirai na kufariki usiku wa Jumatano, Februari 3. Ernest Kamanda anasemekana alianza kukumbwa na matatizo ya kiafya majira ya saa 11:30 jioni Jumatano wakiwa nyumbani kwa mwanamke huyo. 

Kulingana na ripoti ya polisi ambayo TUKO.co.ke iliiona, mwanamke huyo aliyetambulika kama Catherine Kinyanjui mwenye umri wa miaka 47, alikimbizwa katika hospitali ya Shalom akisaidiwa na majirani ambapo alisemakana alikata roho. 

Wiki mbili zilizopita TUKO.co.ke iliripoti kisa ambapo mzee mwenye umri wa miaka 80 aliaga dunia katika njia isiyoeleweka akijivinjari na mrembo wa miaka 33 katika hoteli moja Dar es Salaam, Tanzania. 

David Mluli alipatikana ameaga dunia Jumamosi, Januari 16 katika chumba nambari 22 Mbezi Garden ambapo alikuwa ameenda kufurahia na mrembo kwa jina Neema Kibaya ambaye alikamatwa kutokana na kisa hicho. 
TUTUMIE HABARI,PICHA,MATUKIO AU TANGAZO LAKO TUKUWEKEE KWENYE SHINYANGA PRESS CLUB BLOG,WASILIANA NASI KWA Email : shinyapress@gmail.com Simu/WhatsApp 0756472807