Header Ads Widget

AJALI YA TRENI DODOMA YAUA WATATU NA KUJERUHI 66

Baadhi ya shughuli za utoaji huduma kwa majeruhi zilipokuwa zinafanyika eneo la ajali

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Shirika la Reli Tanzania (TRC) leo Januari 3, 2021, kuhusu ajali ya treni iliyotokea Dodoma, majeruhi ni 66 na waliofariki ni watatu. Kati ya hao watatu mmoja ni mtoto na watu wazima wawili.

Jana Januari 2, 2021 majira ya jioni ilitokea ajali ya treni ya abiria kati ya maeneo ya Itigi, Singida na Bahi, Dodoma.

Majeruhi walipelekwa hospitali na abiria wengine wakafanyiwa utaratibu wa kuendelea na safari zao kwa njia ya mabasi. 

Zaidi soma taarifa kamili ya TRC hapo chini


Post a Comment

0 Comments