Header Ads Widget

WIZARA YA AFYA, WORLD VISION WAZINDUA KITENGO CHA KUTOLEA HUDUMA ZA LISHE HOSPITALI YA MKOA WA SHINYANGA

 
Afisa Lishe Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Saidi Mankiligo (Kushoto) akitoa maelezo kwa mgeni rasmi Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela namna ya kuzingatia mlo kamili na makundi mbalimbali ya vyakula vyenye lishe, wakati wa uzinduzi wa kituo cha kutolea huduma za lishe katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga .

Na Marco Maduhu -Shinyanga
Wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee, na watoto, kwa kushirikiana na Shirika la World Vision, wamezindua kitengo cha kutolea huduma za lishe katika Hospitali ya Rufani Mkoani Shinyanga, ili kutokomeza tatizo la udumavu kwa watoto.
Zoezi la uzinduzi wa kitengo hicho cha kutolea huduma za lishe, limefanyika leo Desemba 11, 2020 katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga na kuambatana na upimaji afya bure kwa wananchi ili kujua afya zao na kupewa elimu ya lishe, huku mgeni Rasmi akiwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, Albert Masovela.

Kaimu Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Lishe kutoka Wizara ya afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Grace Moshi, akizungumza kwenye uzinduzi huo, amesema suala la kuzingatia lishe dhidi ya watoto wadogo ni la muhimu sana na linawajenga kiakili na kiafya.

Amesema mtoto ambaye anazaliwa na udumavu hata kufikili kwake kuna kuwa kwa kiwango cha chini na hawezi kuwa mzuri kwenye masomo yake, tofauti na mtoto ambaye hana udumavu ambapo atakuwa afya ya akili na ndio maana Serikali imeamua kuwekeza kwenye suala la lishe ili kumaliza tatizo la udumavu hapa nchini.

“Wizara ya afya maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto, tutaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa masuala ya lishe, ili kuhakikisha tatizo hili la udumavu hapa nchini linatokomea kabisa, pamoja na magonjwa mengine ambayo yanasababishwa na ulaji vyakula hovyo bila ya kuzingatia lishe bora,”amesema Moshi.

Naye Mkurugenzi wa Miradi kutoka Shirika la World Vision, Nesserian Mollel, amesema Shirika hilo limekuwa likitekeleza miradi ya lishe kwenye wilaya 36 hapa nchini zikiwamo wilaya tatu za mkoa wa Shinyanga, ambazo ni Kishapu, Kahama, Manispaa ya Shinyanga na Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Anasema katika utekelezaji wa mradi huo wa lishe, wana angalia suala la ulinzi na mazingira ya mtoto. elimu ya mtoto, afya ya mtoto, mahusiano mazuri ya mtoto na mazingira, pamoja na kutoa vifaa tiba ambavyo vitasaidia kuboresha huduma za afya.

Kwa upande wake Mgeni Rasmi wa tukio hilo, Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela amesema tatizo la udumavu mkoani humo bado lipo, na hivyo kuwataka wadau wa afya pamoja na watumishi wa Serikali, kuendelea kutoa elimu kwa wananchi tena kwa vitendo, namna ya kuzingatia lishe bora.

Amesema Serikali mkoani humo inaendelea na juhudi za kutokomeza tatizo la udumavu na ndiyo maana kwa sasa wameshazindua zoezi la utoaji wa chanjo ya matone ya Vitamini “A” pamoja na dawa za Minyoo kwa watoto, huku akibainisha kuwa wameshaingia mikataba na wakuu wa wilaya, pamoja na wakurugenzi ili kuhakikisha udumavu una kwisha.

Aidha Afisa Lishe wa Mkoa wa Shinyanga Dennis Madeleke, akizungumza kwa niaba ya Mganga mkuu wa mkoa huo, ametaja hali ya udumavu kuwa ni asilimia 32, na kubainisha kuwa uzinduzi huo wa kitengo cha kutolea huduma za lishe mkoani humo, utasaidia kwa kiwango kikubwa kupunguza tatizo la udumavu.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI


Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela, akizungumza kwenye uzinduzi wa kitengo cha kutolea huduma za lishe kwenye hospitali ya rufani mkoani Shinyanga.

Mkurugenzi msaidizi wa huduma za lishe kutoka wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee, na watoto Grace Moshi, akizungumza kwenye uzinduzi huo wa kitengo cha kutolea huduma za lishe kwenye hospitali ya Rufani Mkoani Shinyanga.

Mkurugenzi wa miradi kutoka Shirika la World Vision Nesserian Mollel, akizungumza kwenye uzinduzi huo wa kitengo cha kutolea huduma za lishe kwenye hospitali ya Rufani Mkoani Shinyanga.

Afisa Lishe wa Mkoa wa Shinyanga, Dennis Madeleke, akizungumza kwa niaba ya Mganga mkuu wa mkoa huo kwenye uzinduzi huo wa kitengo cha kutolea huduma za lishe kwenye hospitali ya Rufani Mkoani Shinyanga.

Mzazi Dina Ibrahimu mkazi wa kijiji cha Wisheteleja wilayani Kishapu akitoa ushuhuda namna elimu ya lishe bora ilivyo okoa afya ya mtoto wake, ambaye alizaliwa akiwa na uzito pungufu.

Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela, (kulia), akiwa kwenye chumba cha kitengo cha kutolea huduma za lishe kwenye hospitali ya Rufani Mkoani Shinyanga, kushoto ni mratibu wa magonjwa yasiyo ya kuambukiza mkoani Shinyanga yatokanavyo na ulaji holela Ruth Kanoni, akipewa vifaa vya kutolea elimu ya lishe bora.

Wananchi wakiwa kwenye uzinduzi wa kitengo cha kutolea huduma za lishe kwenye hospitali ya Rufani Mkoani Shinyanga.

Wananchi wakiwa kwenye uzinduzi wa kitengo cha kutolea huduma za lishe kwenye hospitali ya Rufani Mkoani Shinyanga.

Wananchi wakiwa kwenye uzinduzi wa kitengo cha kutolea huduma za lishe kwenye hospitali ya Rufani Mkoani Shinyanga.

Wananchi wakiwa kwenye uzinduzi wa kitengo cha kutolea huduma za lishe kwenye hospitali ya Rufani Mkoani Shinyanga.

Zoezi la uzinduzi likiendelea.

Zoezi la uzinduzi likiendelea.

Zoezi la uzinduzi likiendelea.

Bango likionyesha ujumbe unaoashiria ufunguzi wa kituo hicho


Katibu tawala wa mkoa wa Shinyanga Albert Msovela, akisikiliza maelekezo ya mlo bora , kwenye uzinduzi wa kitengo cha kutolea huduma za lishe kwenye hospitali ya rufani mkoa wa Shinyanga.

Wananchi wakipata huduma ya kupima afya zao bure, pamoja na kupewa ushauri wa kuzingatia lishe bora, kwenye zoezi hilo la uzinduzi wa kitengo cha kutolea huduma za lishe katika Hospitali ya Rufani Mkoani Shinyanga.

Wananchi wakipata huduma ya kupima afya zao bure, pamoja na kupewa ushauri wa kuzingatia lishe bora, kwenye zoezi hilo la uzinduzi wa kitengo cha kutolea huduma za lishe katika Hospitali ya Rufani Mkoani Shinyanga.

Wananchi wakipata huduma ya kupima afya zao bure, pamoja na kupewa ushauri wa kuzingatia lishe bora, kwenye zoezi hilo la uzinduzi wa kitengo cha kutolea huduma za lishe katika Hospitali ya Rufani Mkoani Shinyanga.


































































































Post a Comment

0 Comments