Header Ads Widget

WATU 14 WAFARIKI KWENYE AJALI SINGIDA



WATI 14 wamepoteza maisha na wengine 13 kujeruhiwa katika ajali ya barabarani iliyotokea mkoani Singida baada ya gari dogo la abiria kugongana uso kwa uso na lori lililokuwa linatoka Dar es Salaam kwenda Kahama.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Sweetbert Njewika, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo katika eneo la Kiini cha Mkiwa kwa kile alichodai ni uzembe wa dereva wa gari la abiria ambaye naye amefariki, aliyekuwa akiendesha kwa mwendo mkali.

Majeruhi wanapatiwa matibabu hospitali ya Manyoni.

Post a Comment

0 Comments