Header Ads Widget

NDUGAI: UKIWA MBUNGE BUBU UMEKWISHA, HAKUNA KUBEBANA


MBUNGE wa Jimbo la Kongwa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Job Ndugai, amechaguliwa kuwa Spika wa Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (2020-2025).

Amechaguliwa kwa 344 kati ya wapiga kura 345 sawa na asilimia 99.7, leo Jumanne, Novemba 10, 2020 bungeni jijini Dodoma.

“Ni kweli kabisa wabunge wengi wa bunge la 12 wanatoka CCM lakini hilo halimaanishi kwamba bunge hili sasa litakuwa la ndiyo, ndiyo, ndiyo wala haimaanishi kwamba bunge hili litakuwa la hapana, hapana, ni bunge ambalo naamini litatekeleza wajibu wake kama ipasavyo.

“Hakuna kubebana, niwape usia wabunge wageni na wengine waliokuwepo, ukichagua kuwa mbunge bubu, usiyesema, unayejipendekeza, husemi chochote, upoupo tu, eti ili uonekane una nidhamu kwenye chama au mahali kwingine umeliwa, usidhani kwamba jambo hilo kwa wananchi wako lina tija, utakuwa umejimaliza kwa wananchi wako.

“Naomba niwaase wabunge wapya na wale waliokuwemo humu, usikubali mtu akukope, bunge lililopita nimepata kesi nyingi sana, mtu anakuja anakulaghai na wewe unakubali, naomba muwe makini sana…” amesema Ndugai ambaye amewahi kuwa Naibu Spika wa Bunge la 10 na Spika wa Bunge la 11.

Post a Comment

0 Comments