Header Ads Widget

MBOWE, LEMA NA JACOB WAACHIWA KWA DHAMANA
Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe

Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe pamoja na wajumbe wa kamati kuu ya chama hicho, Godbless Lema na Boniface Jacob wameachiwa kwa dhamana.
 
Taarifa hiyo imetolewa hii leo Novemba 3, 2020 na Katibu Mkuu wa chama hicho, John Mnyika kupitia ukurasa wake wa 'Twitter'. Awali viongozi hao walishikiliwa na jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam, kwa kosa la kuhamasisha chini kwa chini watu kufanya maandamano bila ya kutoa taarifa kwa Jeshi la polisi.

Post a Comment

0 Comments