Header Ads Widget

'WASHINDI UCHAGUZI MKUU WASHANGILIE BAADA YA KUMALIZA KERO ZA WATANZANIA'


Waumini wa Kanisa la IEAGT Kambi ya Waebrania la Mjini   Shinyanga wakiimba na kumsifu Mungu wakati wa ibada ya Jumapili Oktoba 25, 2020

Na Shinyanga Press Club Blog
WAGOMBEA wanaowania nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano Oktoba 28, 2020 wameaswa kutobweteka baada ya kushinda, bali furaha hiyo ya ushindi waionyeshe baada ya kutatua kero zinazowakabili Watanzania.

 Wito huo umetolewa na Askofu wa Kanisa la International Evangelical Assemblies of God (IEAGT) la mjini Shinyanga, David Mabushi wakati wa ibada ya kihitimisha maombi maalum ya kuombea uchaguzi yaliyofanyika kanisa hapo.

Ambapo, ameshauri kuwa wagombea ili wawe viongozi wa watanzania wanapaswa kutambua kuwa wana jukumu kubwa la kutatua kero za Watanzania kuliko kushangili.

"Uchaguzi ni njia ya kupata watu wenye uwezo wa kusaidia wengine kumaliza kero zao kwani wanapatikana viongozi watakao kuwa na hatma ya kushughulikia kero za taifa hili.

"Ni vyema sana kwa washindi wa uchaguzi kutoshangilia baada ya matokeo bali wajue wana majukumu makubwa sana ya kusaidia Watanzania.....Mtu anayeshangilia ni kuwa hatambui nini maana ya kuwa kiongozi kwa Watanzania," amesema.

Askofu Mabushi amesisitiza kuwa hata matokeo yatakapo tangazwa kwa wale ambao hawajashinda ni vyema wawe na amani na furaha katika mioyo yao kwani walipaswa kubeba majukumu ya kero za Watanzania..
Askofu Mabushi akihubiri kanisani hapo

Post a Comment

0 Comments